Wednesday, December 12, 2012

SODOMA NA GOMORA





HALI ILIVYOBADILIKA MAASI YATENDEKAYO DUNIANI SASA NI ZAIDI YA SODOMA NA GOMORA !!!

·Amuua baba yake na kumkata vipande vipande (Nipashe 14/3/1998)

·Mchungaji afungisha ndoa ya binadamu na mbwa: askofu mkuu Moses Kulola ashuhudia na kulia machozi (Msema kweli 25/11/2001)

·Kaka na dada wadaiwa kutiana mimba wanywa sumu na kufa (Uwazi 26/2 - 4/3.2002)

·Bibi kizee abakwa, anyongwa hadi kufa (Nipashe 23/2/2011)

·Mmarekani adaiwa kumtumia mbwa kumuingilia msichana (Nipashe 7/1/2012)

·Mtoto “amtundika” mimba mama mzazi (Mwananchi 5/6/2012)

·Afumaniwa akifananya mapenzi na mbwa (Majira 12/6/2012)

·Msichana ajisalimisha kanisani kwa kukataa kumtoa kafara mama yake: ni baada ya kuwatoa kafara wadogo zake watano (Msema kweli 5/08/2012)

Mauaji Mwenye Ualbino, Paroko,mganga na baba mbaroni WADAIWA kukutwa na viungo wakisaka mteja ... (Nipashe 20.6.2024)


Hayo hapo juu ni baadhi tu ya matukio machache ya kutisha yaliyowahi kuripotiwa na vyombo vyetu vya habari kwa siku za hivi karibuni, kuonyesha hali ilivyo hapa duniani.


Kumbuka katika matukio kama haya yanayoripotiwa kuna mengine sababu baadhi ya watu huweza kutumia pesa au mbinu nyingine yeyote ili kulinda hadhi ya watu fulani fulani wasiaibishwe pia huweza kumalizwa kifamilia au kindugu ili kuwalinda mtenda na mtendewa.


Kipindi cha Sodoma na Gomora uasi ulipitiliza mpaka walitaka kuwaka malaika wa Mungu, (Mwanzo 19:4 – 22) Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wake waliotoka pande zote, wakamwita Lutu, wakamwambia, wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? uwatoe kwetu tupate kuwajua, Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake, akasema, basi, nawasihi,ndugu zangu msiwatende vibaya hivi. Tazama ninao binti wawili ambao hawajui mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu ... ni mara ngapi hapa nchini kwetu au penginepo duniani umesikia matukio ya ubakaji kwa watoto (Malaika wa Mungu)?


Iwapo Mungu ni yeye yule aliyeleta moto uasi ulivyoongezeka kizazi kile cha Sodoma na Gomora, nini kinachomzuia asilete hukumu kipindi hiki iwapo Mungu ni yeye yule jana na leo na hata milele? Na pia ni yeye asiye na upendeleo? Isije kuwa unasubiriwa wewe peke yako, ndugu kumbuka kuwa neema imefunuliwa sasa kuna muda itafunikwa au itapigwa stop. Kama yule tajiri na maskini Lazaro ambaye alidhani bado ana muda wa kusubiri kidogo (Luka 16:19 -31) Akasema, palikuwa na mtu mmoja, tajiri aliyevaa nguo za zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa, na masikini mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi ...


Dunia inakaribia mwisho na wewe utakuwa wapi? Uamuzi ni wako wewe, na wakati wa kuamua ni sasa si kesho (Mithali 27:1) Usijisifu kwa ajili ya kesho; kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. wokovu unapatikana kwa kumkiri na kumwamini Yesu peke yake na sio mwingine yeyote, hata maandiko yanasema wazi tena kwa lugha ya kueleweka na kila mmoja wetu (Matendo ya mitume 4:22) Si Maria, Si Petro, Si Muhamed, Si Omari, Si Benedict, hawa wote ni binadamu, nao wakifa wataoza na pia watamsubiri huyu Yesu aje awafufue kwa ajili ya uzima au mauti itategemea matendo yao waliyotenda walipokuwa hapa duniani. Maana kila mtu atasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya matendo yake alipokuwa hapa duniani (Warumi 14:12) Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.


Hukumu ya mwisho, kiyama na itakuja ghafla kwa hiyo ni bora uwe tayari wakati wowote ili ukikutwa sehemu yoyote ile utwaliwe (Mathayo 24:40-42) Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa,mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 


Tufanye kazi, tusome na shughuli nyingine zote kwa bidii sana lakini tusimsahau Mungu wetu , kwani kifo kwangu au kwako kinaweza kuja kwa ghafla, nitakuwa au utakuwa wapi milele? Na kuongoka, kuokoka, kuzaliwa upya, kumwamini Bwana Yesu Kristo ni hapa hapa duniani, si baada ya kufa (Waebrania 9:27) Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. baadhi ya watu walio okoka wakiwa hapa hapa duniani pamoja na ufalme,utajiri,ubabe wao walimkubari Yesu (Matendo ya mitume 9:1-16 Paulo-mbabe)Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, akataka ampe barua za kwenda Dameski, zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa njia hii,waume kwa wake, awafunge, na kuwaleta Yerusalemu ...  (Luka 19:1-10 Zakayo-tajiri) Naye alipoingia Yeriko alipita kati kati yake. Na tazama palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri ... (Mwanzo 6:13-17 Nuhu) Mungu akamwambia Nuhu, mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia. Ujifanyie safina ya mti wa mvinje: fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami ...

Kuokoka , kuongoka, kuzaliwa mara ya pili, kumwamini Bwana Yesu Si kuchanganyikiwa,Si kulia lia,Si ku fell ki maisha,Si kuwa zezeta, Si kuwa masikini, Si kuwa mchafu mchafu,Si kushinda kanisani muda wote, kama shetani anavyosambaza tafsili yake ya kuokoka, kuokoka ni kumwamini Yesu na kukubali kuwa alikufa msarabani kwa ajili yetu, yaani kifo chake pale msarabani hakikuwa kazi bure, ilikuwa kwa ajili yangu mimi na wewe atupate, una surrender na kuanzia hapo unafanya maamuzi hayo magumu kwa baadhi ya watu. Baada ya hapo unaishi kwa kuifuata BIBLE“Basic Intructions Before Living in Earth”


Kama utakuwa na utayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.


“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”


Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.

1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku. (Warumi 10:17), (Wakolosai 3:16)

2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike   5:17)

3.Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri wokovu na kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25)

4. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani. (Ufunuo 3:11), ( Mwanzo 3:1-19) (1Petro 5:8)

5. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) ,( Kolosai 4:16)

                                                                    Ni mimi

Mtumishi Emmanuel T. M.Omari
injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com





No comments:

Post a Comment