Watu wakiwa katika ibada ya sanamu
MUNGU AMESINZIA, AMELALA AU HAONI?
Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione? (Zaburi 94:9)
Hapa naomba tusaidiane ndugu zangu sijui wewe unamwabudu nani? Au nini? na Mungu anasemaje katika maandiko yake, (Kutoka 20:4-6) Wa kumwabudu ni Mungu Jehova/Niko ambaye niko, yahwe, peke yake, hakuna mwingine. Si mnyama simba, Si tembo,Si nyangumi wala si binadamu Juma, Si Yohana, Si Muhamed, Si Petro n.k wala si kitu mf.jua, jabali,mwezi wala nyota.
Kwa hiyo mitume na manabii, maaskofu, makasisi, wachungaji, watabiri, hawa wote ni binadamu watakufa na kuoza na kubakia mifupa, ila kwa uwezo wa Mungu watafufuliwa siku ya mwisho ni kitendo cha dakika moja kufumba na kufumbua (1Korintho 15:52) kwa ajili ya ujio wa Yesu ili wapokee malipo yao kila mtu kutokana na matendo aliyotenda alipokuwa hapa duniani. Kama alitenda mema atalipwa na uzima wa milele kama alitenda mabaya atapata hukumu ya milele. (Warumi 2:6-9)
Sijui umewahi kujiuliza swali hili lifuatalo, Watu wanao ua au kuwatesa watu wengine bila hatia kwa siri au kwa dhahiri, wachawi kwa kutoa misukule na majambazi kuiba na kuua na Wengine wanatesa wasichana wa kazi na kuwafanyia matendo yasiyo sawa mbele za Mungu yote haya huweka rekodi siku ya siku yote yatafunuliwa na kuwa wazi (Waebrania 4:13) Hakuna cha kujificha mbele za Mungu na (Zaburi 139:7,8).
mafisadi hayo matendo yao, je Mungu anayeona kila mahali amelala au amesinzia au haoni na kuchukua hatua mara moja yeye si wa haki yote?
(Warumi 2:4), Mungu anakuvumilia/anawavumilia akiamini kuwa itafika siku utaacha matendo mabaya na kumgeukia yeye.
Pia sisi kama binadamu suala la kulipa kisasi si letu ni la Mungu yeye atalipa kwa haki anaweza kukulipa kuanzia hapa duniani na mwisho siku utakaporudi kwake tena itakuwa milele na milele (Warumi 12:19) duniani hapa si makazi ya kudumu ni wapitaji tu kama maua leo tupo kesho hatupo.(Ayubu 14:1-2)
Mungu yeye ni wa rehema haoni hasira upesi anawapa muda wale wote wanaofanya machukizo mbali mbali waache mara moja pamoja na kuwa wanatumia hewa yake, anataka wote watubu (Ufunuo 2:16) na pia anakuja upesi (Ufunuo 3:11)
Binadamu tuna kawaida ya kuweka kamera fulani kwa ajili ya usalama sehemu mbali mbali kwa ajili ya ulinzi matukio yote mabaya na mazuri hurekodiwa iwe usiku au mchana huchukuliwa na mitambo hii na kuhifadhiwa baadaye huweza kufuatiliwa kwa shari au kwa wema, Mungu ni muweza yote matukio yote tuyafanyayo kwa kuzani kuwa Mungu hatuoni kuna siku yote yatawekwa wazi na kuhukumiwa kutokana na matendo yetu (Warumi 14:11) kwa kuwa yeye alituumba na kutupachika macho lazima awe zaidi katika kuona, alitupachika sikio lazima awe na uwezo uliotuzidi katika kusikia, siku hizi tena teknolojia ipo juu kiasi kwamba kuna kamera zinarekodi matukio yanayofanyika mchana kweupe na nyingine zinarekodi matukio yanayoweza fanyika usiku kwenye giza, huoni kuwa lazima Mungu atakuwa na uwezo zaidi yetu sisi? utafanya jambo gani ovu ili kumficha Mungu muumbaji wa vitu vinavyo onekana na visivyo onekana.
Mungu hana upendeleo huwa anaongea na wote wafanyao hayo maovu akiwasihi waache kwa kuwapa misuko suko fulani kama fundisho kwao, hata ujumbe kama huu inaweza kwako ikawa ni sauti ya Mungu ikitaka mambo hayo ya kinyama uyafanyayo uyaache na kumrudia Mungu, kama hutakubari basi. Wakati mwingine Mungu hutumia mahubiri ya watumishi wa Mungu mbali mbali kwa kutumia radio, mikutano ya kiroho, vipeperushi,bado unakuwa hutaki kuacha, Lazaro alipokufa alichukuliwa kifuani kwa Mungu ila yule tajiri alifika mahali pa mateso akatamani kurudi duniani awaambie ndugu zake Mungu akasema wanao Musa na manabii (Luka 16:29) Mungu huwa anasema ukitii utakula mema ya nchi maana yake usipotii hutakula mema hayo, pia neno la Mungu likowazi linasema mshahara wa dhambi ni mauti Mungu anajua wapi pa kupeleka mashambulizi za hiyo mauti anayoiongelea. Mungu hafundishwi na Mtu yeye anajua yote na anaweza yote.
Mungu ana kawaida ya kumwambia mtu kwa njia mbali mbali kama utakuwa mbishi kupitiliza atakuacha na akikuacha maana yake unakuwa halali ya shetani unakuwa chini ya laana bila kujijua. (Mithali 29:1), na atakuwa anajifariji kwa mahubiri ya shetani ambayo nayo ni injili nyingine inayompeleka mtu katika laana ya milele (Wagalatia1:8-9)
Watu wamekuwa wakifanya maovu mbali mbali kama kwamba Mungu amesinzia, amelala au haoni na sababu ya mambo kama hayo huweza kushusha ghadhabu ya Mungu kwa wanadamu na taifa na hata dunia yote, wakati mwingine Mungu husubiri labda huyu mtu atageuka pia huofia kupiga dunia pamoja na wema (Mwanzo 18:23-33) ingawa wakati mwingine huweza kuruhusu balaa Fulani limpate yeye aliye fanya tu. Ahimidiwe Mungu mwenye haki, amesema roho ya yeye atendaye dhambi ndiyo itakayo kufa, uzinzi mshahara wake ukimwi baadaye moto wa milele, mwizi mshahara wake kuchomwa moto baadaye adhabu ya milele, kuiba wake za watu mshahara wake kufumaniwa na kudhalilishwa, ingawa hapa kuna watu wengine huwasukumia kesi watu wengine mtu anaweza kufanya uovu fulani kwa kutumia cheo chake anaweza akabambikiwa kesi asiyehusika ili kumlinda mtu fulani, Mungu yote haya anayaona.
Ulimwengu huu tunaoishi una mwisho wake duniani hapa ni wapitaji tu hatuna muda mrefu wa kuishi sana sana unaweza kufikia labda miaka 60 au 80 au 100, baada ya kufa maisha yatakuwa ni milele umejiandaliaje umilele wako? Mwamini Yesu tembea naye kama akiba na kumtumikia kwa bidii, siku hizi maadui wa uhai wa mtu ni wengi mno karibu kila kitu hakina usalama hofu na mashaka vimeongezeka mno kuliko kawaida.Ajali nyingi siku hizi, magonjwa mengi, vita visivyoisha duniani,uchawi tena una advance kila kukicha, upo mpaka wa kununua, usalama wetu upo wapi?
Mkimbilie Yesu uwe salama uwe naye sasa ukimtumikia na kama utakufa kabla ya kuchukuliwa kwa kanisa utakuwa unaenda kula faida au matunda ya utumishi.(Wafilipi 1:21)
Watu wengine hudhani kuwa mtu anapokufa ndio safari imeishia hapo katika mwili huo ni uongo wa shetani na mawakala wake, ndio maana watu wengine matatizo yanapowasibu asione pa kutokea huchukua uamuzi wa kipuuzi wa kujinyonga, ili apotelee mbali. Asikudanganye mtu yeyote ukifa ndio umeanza safari nyingine ya kuelekea nyumbani kwetu kwa milele ambako yatahusisha mwili wa roho mwili huu wa udongo tutauacha hapa duniani, maisha yako kuwa mazuri au mabaya itategemea uliishi vipi ulipokuwa hapa duniani, Muulize yule tajiri na masikini Lazaro, uone pia jinsi masikini alivyopewa heshima hata tu kwa kulitaja jina lake Lazaro, ila tajiri hakutajwa jina maana umaarufu wake ulikuwa huko duniani, na maisha yake yaliishia kikomo alitamani arudishwe tena duniani aanze moja ikashindikana kabisa, akamwomba Mungu atoke mtu kutoka kuzimu ashuhudie mateso, harafu akawaambie watu waishio duniani Mungu akasema hapana! Wanao Musa na manabii na wawasilize hao.(Luka mt 16:19-31).Hata hivyo kutokana na ombi la yule tajiri, kuna baadhi ya watu mbali mbali walishawahi kuchukuliwa na Yesu mwenyewe kwenda kuzimu na kurudi hapa duniani ili kushuhudia, japo kwa uchache mambo ya huko.
Pia kuna baadhi ya watumishi wa Mungu hufuatwa na kupewa kipawa cha kufanya miujiza ya kutisha ila ni nguvu kutoka upande ule wa adui wakipewa masharti wafanye miujiza lukuki ila si kuwahubiri watu habari za wokovu kuachana na zambi na huku wakiahidiwa kupewa mishiko (pesa) ya nguvu, na watu hao mawakala wa shetani, hapa sina maana miujiza yote inayofanyika kwenye nyumba za ibada inatoka kwa shetani ole kwa watumishi. Shetani hawapendi watu waliokombolewa. Sababu kuu ni kuwa wanafanya baadhi ya kazi zake zivurugike, maana wakati mwingine watu waliokombolewa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu huweza kugundua hila mbali mbali na makusudio yake aliyoipanga kwa wanadamu. Kama tujuavyo kuwa mipango mingi na mikakati mbali mbali ya shetani ilianzia kama maazimio katika vikao na kutoa maamuzi kwamba iwe hivi au vile, ili shetani atukuzwe. Ingawa watu wa Mungu nao kabla ya mikakati mbali mbali pia huanza kwa maazimio mbali mbali mfano:tufanye mkutano wa injili sehemu fulani ili watu wamgeukie Mungu wa kweli. Tukatembelee wagonjwa katika hospitali fulani
Mungu anawatafuta watu wanaotaka kumwabubu yeye katika roho na kweli kila siku, anza maisha mapya kwa kumkiri/ kumwamini Yesu/ kuongoka leo usisubiri kesho. (Mithali 27:1)
FANYA MAAMUZI BINAFSI YA KUMKUBARI YESU PEKEE KWA AJILI YA WOKOVU
Sali Sala ifuatayo kwa kumaanisha, tafuta mahali pa utulivu usali Mungu yupo kila mahali, (Yohana mt 4:24), hakuna mahali utakapokuwa Mungu asiwepo (Zaburi 139:7-8).
SALA:
“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”
Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.
1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku Warumi 10:17, Wakolosai 3:16
2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. Wathesalonike 5:17
3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri wokovu na kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. 1Petro 2:1-2, Waebrania 10:25. 4. Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione aibu, acha uvivu, tafuta pesa, Mungu katoa agizo tangu kale, Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo hivyo ( 2Thesalonike 3:10)
5. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani Ufu 3:11, Mwanzo 3:1-19 na 1Petro 5:8
6. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.Ufunuo 22:18 , Kolosai 4:16 Ni mimi
Mtumishi Emmanuel T.M.Omari injiliyajioni@gmail.com www.injilijioni.blogsport.com | |
Yohana Mtakatifu 9:4 Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.
Tuesday, December 11, 2012
MUNGU AMESINZIA, AMELALA AU HAONI ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment