Wednesday, December 12, 2012

SODOMA NA GOMORA





HALI ILIVYOBADILIKA MAASI YATENDEKAYO DUNIANI SASA NI ZAIDI YA SODOMA NA GOMORA !!!

·Amuua baba yake na kumkata vipande vipande (Nipashe 14/3/1998)

·Mchungaji afungisha ndoa ya binadamu na mbwa: askofu mkuu Moses Kulola ashuhudia na kulia machozi (Msema kweli 25/11/2001)

·Kaka na dada wadaiwa kutiana mimba wanywa sumu na kufa (Uwazi 26/2 - 4/3.2002)

·Bibi kizee abakwa, anyongwa hadi kufa (Nipashe 23/2/2011)

·Mmarekani adaiwa kumtumia mbwa kumuingilia msichana (Nipashe 7/1/2012)

·Mtoto “amtundika” mimba mama mzazi (Mwananchi 5/6/2012)

·Afumaniwa akifananya mapenzi na mbwa (Majira 12/6/2012)

·Msichana ajisalimisha kanisani kwa kukataa kumtoa kafara mama yake: ni baada ya kuwatoa kafara wadogo zake watano (Msema kweli 5/08/2012)

Mauaji Mwenye Ualbino, Paroko,mganga na baba mbaroni WADAIWA kukutwa na viungo wakisaka mteja ... (Nipashe 20.6.2024)


Hayo hapo juu ni baadhi tu ya matukio machache ya kutisha yaliyowahi kuripotiwa na vyombo vyetu vya habari kwa siku za hivi karibuni, kuonyesha hali ilivyo hapa duniani.


Kumbuka katika matukio kama haya yanayoripotiwa kuna mengine sababu baadhi ya watu huweza kutumia pesa au mbinu nyingine yeyote ili kulinda hadhi ya watu fulani fulani wasiaibishwe pia huweza kumalizwa kifamilia au kindugu ili kuwalinda mtenda na mtendewa.


Kipindi cha Sodoma na Gomora uasi ulipitiliza mpaka walitaka kuwaka malaika wa Mungu, (Mwanzo 19:4 – 22) Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wake waliotoka pande zote, wakamwita Lutu, wakamwambia, wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? uwatoe kwetu tupate kuwajua, Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake, akasema, basi, nawasihi,ndugu zangu msiwatende vibaya hivi. Tazama ninao binti wawili ambao hawajui mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu ... ni mara ngapi hapa nchini kwetu au penginepo duniani umesikia matukio ya ubakaji kwa watoto (Malaika wa Mungu)?


Iwapo Mungu ni yeye yule aliyeleta moto uasi ulivyoongezeka kizazi kile cha Sodoma na Gomora, nini kinachomzuia asilete hukumu kipindi hiki iwapo Mungu ni yeye yule jana na leo na hata milele? Na pia ni yeye asiye na upendeleo? Isije kuwa unasubiriwa wewe peke yako, ndugu kumbuka kuwa neema imefunuliwa sasa kuna muda itafunikwa au itapigwa stop. Kama yule tajiri na maskini Lazaro ambaye alidhani bado ana muda wa kusubiri kidogo (Luka 16:19 -31) Akasema, palikuwa na mtu mmoja, tajiri aliyevaa nguo za zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa, na masikini mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi ...


Dunia inakaribia mwisho na wewe utakuwa wapi? Uamuzi ni wako wewe, na wakati wa kuamua ni sasa si kesho (Mithali 27:1) Usijisifu kwa ajili ya kesho; kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. wokovu unapatikana kwa kumkiri na kumwamini Yesu peke yake na sio mwingine yeyote, hata maandiko yanasema wazi tena kwa lugha ya kueleweka na kila mmoja wetu (Matendo ya mitume 4:22) Si Maria, Si Petro, Si Muhamed, Si Omari, Si Benedict, hawa wote ni binadamu, nao wakifa wataoza na pia watamsubiri huyu Yesu aje awafufue kwa ajili ya uzima au mauti itategemea matendo yao waliyotenda walipokuwa hapa duniani. Maana kila mtu atasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya matendo yake alipokuwa hapa duniani (Warumi 14:12) Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.


Hukumu ya mwisho, kiyama na itakuja ghafla kwa hiyo ni bora uwe tayari wakati wowote ili ukikutwa sehemu yoyote ile utwaliwe (Mathayo 24:40-42) Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa,mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 


Tufanye kazi, tusome na shughuli nyingine zote kwa bidii sana lakini tusimsahau Mungu wetu , kwani kifo kwangu au kwako kinaweza kuja kwa ghafla, nitakuwa au utakuwa wapi milele? Na kuongoka, kuokoka, kuzaliwa upya, kumwamini Bwana Yesu Kristo ni hapa hapa duniani, si baada ya kufa (Waebrania 9:27) Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. baadhi ya watu walio okoka wakiwa hapa hapa duniani pamoja na ufalme,utajiri,ubabe wao walimkubari Yesu (Matendo ya mitume 9:1-16 Paulo-mbabe)Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, akataka ampe barua za kwenda Dameski, zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa njia hii,waume kwa wake, awafunge, na kuwaleta Yerusalemu ...  (Luka 19:1-10 Zakayo-tajiri) Naye alipoingia Yeriko alipita kati kati yake. Na tazama palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri ... (Mwanzo 6:13-17 Nuhu) Mungu akamwambia Nuhu, mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia. Ujifanyie safina ya mti wa mvinje: fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami ...

Kuokoka , kuongoka, kuzaliwa mara ya pili, kumwamini Bwana Yesu Si kuchanganyikiwa,Si kulia lia,Si ku fell ki maisha,Si kuwa zezeta, Si kuwa masikini, Si kuwa mchafu mchafu,Si kushinda kanisani muda wote, kama shetani anavyosambaza tafsili yake ya kuokoka, kuokoka ni kumwamini Yesu na kukubali kuwa alikufa msarabani kwa ajili yetu, yaani kifo chake pale msarabani hakikuwa kazi bure, ilikuwa kwa ajili yangu mimi na wewe atupate, una surrender na kuanzia hapo unafanya maamuzi hayo magumu kwa baadhi ya watu. Baada ya hapo unaishi kwa kuifuata BIBLE“Basic Intructions Before Living in Earth”


Kama utakuwa na utayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.


“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”


Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.

1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku. (Warumi 10:17), (Wakolosai 3:16)

2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike   5:17)

3.Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri wokovu na kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25)

4. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani. (Ufunuo 3:11), ( Mwanzo 3:1-19) (1Petro 5:8)

5. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) ,( Kolosai 4:16)

                                                                    Ni mimi

Mtumishi Emmanuel T. M.Omari
injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com





Tuesday, December 11, 2012

WEWE INGIA KULIA, WEWE NENDA KUSHOTO



    WEWE PITA UINGIE KUSHOTO UNASTAHILI, WEWE PITA UINGIE KULIA UNASTAHILI !!!


Hii itakuwa ni amri ambayo haitakuwa na mjadala,ujanja ujanja, ubaunsa wa kupitiliza kuwazidi malaika wa Mungu na Mungu mwenyewe kama vile ilivyo ngumu kuzuia kifo basi katika tukio hili kutakuwa hamna ujanja ujanja.
Kipindi cha Nuhu watu au binadamu wa wakati ule waliambiwa watengeneze njia zao kwa kumrudia Mungu lakini walimuona Nuhu kuwa kama amechanganyikiwa, hana pesa,mlokole, hajasoma, masikini mkubwa, wengine walimtukana, wakawa wakiendelea kuponda starehe wengine wakijenga majumba kila kukicha. Ndivyo ilivyo hata leo injili inahubiriwa karibu kila kona ya dunia mahospitalini, vituoni mwa dala dala, katika maeneo ya wazi, lakini matokeo yake wahubiri hawa huishia kutukanwa, kuonekana kuwa kama wamechanganyikiwa na dini, hawana pesa,hawana elimu ya kutosha, wamekosa kazi za kufanya.

 

Watu wa kizazi kile cha Nuhu walitegemea ujuzi wao wa kuogelea, baada ya kuambiwa jamani tumrudie Mungu kwani tusipomrudia tutaangamizwa kwa mvua kubwa, ah! Wapi siku ya siku walioweza kuogelea walijitahidi mpaka katika mlango wa safina, lakini mlango haukuweza kufunguka maana aliye funga mlango alikuwa ni Mungu mwenyewe (Mwanzo 7:16).Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyoamuru Mungu; Bwana akamfungia.
Mungu katika maandiko yake amesema sitaiadhibu dunia tena kwa maji (Mwanzo 8:21) Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitaipiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. Mungu anaposema sitaadhibu tena kwa maji maana yake adhabu ipo, Mungu ni wa nuruni hakuficha katika sehemu nyingine katika maandiko yake amefunua wazi adhabu itakuwa ya namna gani (Marko 9:43-48) Na mkono wako ukikukosesha,ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu kuliko, kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanam, kwenye moto usiozimika; (ambao humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki) Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanam; ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.


 


Pia tunamuona Mungu akiwaagiza Adam na Eva wasile tunda katika katika mti wa katikati ya bustani hapa Mungu alikuwa anaagiza kwamba wasifanye dhambi ila watii sheria ili waende sawa, ila tunamuona shetani (Nyoka) aliyejaa hila na udanganyifu akiwapotosha ili watu hawa wamkosee Mungu wasifikie malengo ambayo Mungu alikuwa amewawekea, kama alivyofanya hila kipindi cha wazazi wetu (Adam na Eva ) wakakosea ndiyo hila hiyo hiyo anayoitumia katika kizazi hiki kwa kuleta dini na madhehebu lukuki mengine ya uongo na mengine ya ukweli na watumishi wa Mungu ambao wengine sio bali ni wa Shetani, ila wanavaa mavazi ya kondoo, bila msaada wa Roho mtakatifu ni ngumu kuwatambua maana na wao wanaitumia biblia hii takatifu,na wanafanya miujiza kwa jina la yesu, ila hawamtaji yesu yupi, katika biblia kuna yesu wengi (Matendo 13:7) Walipopita katikati ya kisiwa chote mpaka pafo, wakaona mtu mmoja,mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu. ndio maana wakati Yesu alipokuwa akiondoka alituachia Roho Mtakatifu bila huyo sijui ingekuwaje! maana hawa watu wanaojiita watumishi wa Mungu si wa Mungu ila ni wa mungu wa dunia hii (2 Wakorinto 4:4) Ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


Sisi je! Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii bila kumkimbilia Yesu (Waebrania 2:3) Sisi je! tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia.  ambaye peke yake ndie mwenye uwezo wa kutufikisha kwa Mungu na sio mwingine yeyote awe nabii aumtume au kuhani au mwalimu au profesa au mtabiri ambaye akifa ni kuoza tu. (Matendo 4:12).Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Baada ya Wazazi wetu kufanya kosa kila mmoja alipata adhabu yake nyoka kutembea kwa tumbo, mwanamke kuzaa kwa uchungu na mwanamme kula kwa jasho lake sababu yeye Mungu hana upendeleo kila mtu atahukumiwa kutokana na matendo yake.
Nini maana ya dini, dini ni mpango wa mwanadamu wa kumtafuta Mungu au mungu uamuzi ni wake binafsi.

 

Wokovu ni mpango wa Mungu wa kumtafuta mwanadamu ili aje katika kusudi lake (Yoh 3:16) Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Wewe upo njia ipi? Duniani hapa njia zipo nyingi mpaka mtu unaweza kuchanganyikiwa njia za Mungu wa kweli na mungu wa uongo humo humo ni michanganyo tu, ni kipindi ambacho Yesu alitabiri juu yake akisema siku za mwisho aliposema, nyakati za mwisho kutatokea makristo na manabii wengi wa uongo. (Mathayo mt 24:11) Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi
Kama ilivyo kwa Mungu kwa kuwa anazo nguvu na shetani naye anavyo vi guvu, kila upande unamvuta mwanadamu aje kwake, hapa sasa itategemea hiyari ya huyo mtu anayetakiwa na kila upande.Mungu ndiye muumbaji ana uchungu na watu wake ndio maana kwa gharama yeyote anawaangaikia, twende kwake ili tupate uponyaji, shetani yeye hana uchungu anasubiria hukumu, kiboko chake na kila siku anajitahidi watu waje kwake ili kuongeza idadi ya wafuasi ambao ataenda nao motoni, ingawa ule moto ni kwa ajili ya shetani na malaika zake binadamu ataingia katika janga hili kwa kujitakia tu (Mathayo 25:41) tena wakati mwingine akikisia huyu anataka kuniacha anaweza akamuondoa duniani halaka halaka ili akose nafasi ya kutubu kabisa awe anasubiria hukumu tu, sababu shetani anajua ukisha maliza kifo utakuwa unasubiria hukumu tu, pia anawatajilisha kwa utajili huu wa duniani ambao una mwisho unatajirika kwa kuwa ana kila kitu cha hapa duniani, ila mambo ya mbinguni hata a,e,i,o,u yake hujui.
Mitume, manabii, walimu, maprofesa, wachungaji wote waliokwisha kufa wamekufa nao wanasubulia hukumu yao siku ya mwisho kama walifundisha uongo watapata malipizo yao na adhabu ya milele kwa moto wa jehanam na kama walifundisha mema watapata thawabu yao, kila mtu atalipwa kutokana na matendo yake au kila mtu atavuna kile alichopanda. Na Yesu ndiye atakaye rudi siku ya mwisho si mwingine yeyote, wote wamelala mpaka siku ya mwisho, hapo ndio itakuwa ni kizaa zaa hakuta kuwa na muda tena wa kusikia habari za injili neema itakuwa imefungwa, maana sasa hivi neema hii ipo wazi, imefunuliwa kwa watu wote, kuna muda unakuja itafunikwa, itapigwa stop. (Tito 2:11) Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa.  Sijui itakuwa vipi ndugu yangu, je utaamua kesho ? unajua ya kesho wewe Mungu amekupangia nini? (Mithali 27:1) Usijisifu kwa ajili ya kesho; kwa maana hujui yatakayo zaliwa na siku moja.
Unaweza kujiuliza hivi, hivi kwa nini Mungu asingeruhusu watu wapenye yaani waende bure bure tu, Mungu hana upendeleo kwa Yesu ukombozi ulimghalimu nawe pia lazima uchangie gharama,sababu wewe upo upande wa Mungu yeye alichangia, Yesu alichangia, Roho Mtakatifu alichangia kwa nini wewe usichangie? hujui kuwa uliumbwa kwa mfano wa Mungu ?na vile vile Mungu hapendi watu wapate kitu bure bure, hata Adamu na Eva Mungu aliwapa bustani/shamba walime, alikuwa na uwezo wa kuwapa chakula bure, ila si utaratibu wa Mungu kupata kitu bura bure tu, ukienda kinyume na maagizo yake utakuwa unamtenda dhambi, pia Mungu hana upendeleo. Mungu hataki watu wavivu anataka kila kitu ukifanyie kazi, aliumba dunia kwa siku sita siku ya saba akapumzika wewe ni nani usiye taka kufanya kazi, Kama Mungu alivyo nasi pia tupo hivyo hivyo.
Mungu ni mpole sana, tena ni mkali sana, tena anatupenda sana, tena ana hasira sana juu yao wote watendao mambo maasi, hacheki na dhambi Mungu anaangalia neno lake apate kulitimiza, haendi kinyume na alivyosema pia hana kigeu geu, ikiwa alisema atatimiza. Kama alisema Yesu atarudi mara ya pili atarudi kweli si uongo, hata kama atachelewa atarudi.

 

Mungu anapoona mtu yeyote hata kama anatoa sadaka sana, anasali sana ana huruma sana haisaidii sana kukufanya uwe na sifa ya kwenda mbinguni kwake, lazima umkiri huyu Yesu upate msamaha na ondoleo la dhambi uwe na tiketi ya kumuona mwokozi, vinginevyo siku ya siku utaishia wewe pia pita huko kushoto unasthahili, malaika wakikusindikiza bila kuwa na la kujitetea.
Kama utahitaji kuepuka balaa hilo, la kuikosa mbingu ambapo hata viongozi wetu wa dini nao watakuwa wanasubiri katika zamu zao wakisubiri mishahara yao hawataweza kumtetea mtu awaye yote. Watasimama mbele za Mungu wakitoa hesabu ya matendo yao (Warumi 14:12) Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
Mbegu hupandwa ikafa na kuleta mmea mwingine mpya mzuri, ndivyo hivyo miili yetu ya udongo itakuwa ilisha kufa na kuoza na kuinuliwa tukiwa na miili mingine ya kiroho au ya kimbingu mbingu.
Kama utapenda kujiunga na wanao mwamini Yesu tafuta mahali palipo tulia na kufuatisha maneno ya sala hii iliyoandikwa, uisome kwa kumaanisha baada ya kumaliza maneno ya sala hii utakuwa umemkaribisha Yesu ndani ya moyo wako naye atakuwa wako (Warumi 10:9) Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.  pia hata kuacha mpaka mwisho wa dunia, ila pia kama hutakuwa tayari ni wewe mwenyewe sasa maana wokovu kumwamini Yesu si lazima ni hiyari, maana Mungu humpenda yeye afanyaye mambo yake bila kulazimishwa.(2Wakoritho 9:7)
Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye (moyo) kwa moyo wa ukunjufu.

SALA 

“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi. Sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha.....(zitaje mbele za Mungu) niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.” Amen

Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.


1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku (Warumi 10:17),  (Wakolosai 3:16)
2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike 5:17)
3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri wokovu        na kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25).
4. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani (Ufu 3:11), (Mwanzo 3:1-19 )na (1Petro 5:8)
5. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji          ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) , (Kolosai 4:16).


                            Ni mimi


               Mtumishi Emmanuel T.M.Omari
                injiliyajioni@gmail.com
                www.injilijioni.blogsport.com

 





MUNGU AMESINZIA, AMELALA AU HAONI ?




                             
  
 
Watu wakiwa katika ibada ya sanamu

MUNGU AMESINZIA, AMELALA AU HAONI?

Aliyelitia sikio mahali pake asisikie? Aliyelifanya jicho asione? (Zaburi 94:9)

Hapa naomba tusaidiane ndugu zangu sijui wewe unamwabudu nani? Au nini? na Mungu anasemaje katika maandiko yake, (Kutoka 20:4-6) Wa kumwabudu ni Mungu Jehova/Niko ambaye niko, yahwe, peke yake, hakuna mwingine. Si mnyama simba, Si tembo,Si nyangumi wala si binadamu Juma, Si Yohana, Si Muhamed, Si Petro n.k wala si kitu mf.jua, jabali,mwezi wala nyota.

Kwa hiyo mitume na manabii, maaskofu, makasisi, wachungaji, watabiri, hawa wote ni binadamu watakufa na kuoza na kubakia mifupa,  ila kwa uwezo wa Mungu watafufuliwa siku ya mwisho ni kitendo cha dakika moja kufumba na kufumbua (1Korintho 15:52) kwa ajili ya ujio wa Yesu ili wapokee malipo yao kila mtu kutokana na matendo aliyotenda alipokuwa hapa duniani. Kama alitenda mema atalipwa na uzima wa milele kama alitenda mabaya atapata hukumu ya milele. (Warumi 2:6-9)

Sijui umewahi kujiuliza swali hili lifuatalo, Watu wanao ua au kuwatesa watu wengine bila hatia kwa siri au kwa dhahiri, wachawi kwa kutoa misukule na majambazi kuiba na kuua na Wengine wanatesa wasichana wa kazi na kuwafanyia matendo yasiyo sawa mbele za Mungu yote haya huweka rekodi siku ya siku yote yatafunuliwa na kuwa wazi (Waebrania 4:13) Hakuna cha kujificha mbele za Mungu na (Zaburi 139:7,8).

mafisadi hayo matendo yao, je Mungu anayeona kila mahali amelala au amesinzia au haoni na kuchukua hatua mara moja yeye si wa haki yote?

(Warumi 2:4), Mungu anakuvumilia/anawavumilia akiamini kuwa itafika siku utaacha matendo mabaya na kumgeukia yeye.

Pia sisi kama binadamu suala la kulipa kisasi si letu ni la Mungu yeye atalipa kwa haki anaweza kukulipa kuanzia hapa duniani na mwisho siku utakaporudi kwake tena itakuwa milele na milele (Warumi 12:19) duniani hapa si makazi ya kudumu ni wapitaji tu kama maua leo tupo kesho hatupo.(Ayubu 14:1-2)

Mungu yeye ni wa rehema haoni hasira upesi anawapa muda wale wote wanaofanya machukizo mbali mbali waache mara moja pamoja na kuwa wanatumia hewa yake, anataka wote watubu (Ufunuo 2:16) na pia anakuja upesi (Ufunuo 3:11)

Binadamu tuna kawaida ya kuweka kamera fulani kwa ajili ya usalama sehemu mbali mbali kwa ajili ya ulinzi matukio yote mabaya na mazuri hurekodiwa iwe usiku au mchana huchukuliwa na mitambo hii na kuhifadhiwa baadaye huweza kufuatiliwa kwa shari au kwa wema,  Mungu ni muweza yote matukio yote tuyafanyayo kwa kuzani kuwa Mungu hatuoni kuna siku yote yatawekwa wazi na kuhukumiwa kutokana na matendo yetu (Warumi 14:11) kwa kuwa yeye alituumba na kutupachika macho lazima awe zaidi katika kuona, alitupachika sikio lazima awe na uwezo uliotuzidi katika kusikia, siku hizi tena teknolojia ipo juu kiasi kwamba kuna kamera zinarekodi matukio yanayofanyika mchana kweupe na nyingine zinarekodi matukio yanayoweza fanyika usiku kwenye giza, huoni kuwa lazima Mungu atakuwa na uwezo zaidi yetu sisi? utafanya jambo gani ovu ili kumficha Mungu muumbaji wa vitu vinavyo onekana na visivyo onekana.

Mungu hana upendeleo huwa anaongea na wote wafanyao hayo maovu akiwasihi waache kwa kuwapa misuko suko fulani kama fundisho kwao, hata ujumbe kama huu inaweza kwako ikawa ni sauti ya Mungu ikitaka mambo hayo ya kinyama uyafanyayo uyaache na kumrudia Mungu, kama hutakubari basi.  Wakati mwingine Mungu hutumia mahubiri ya watumishi wa Mungu mbali mbali kwa kutumia radio, mikutano ya kiroho, vipeperushi,bado unakuwa hutaki kuacha, Lazaro alipokufa alichukuliwa kifuani kwa Mungu ila yule tajiri alifika mahali pa mateso akatamani kurudi duniani awaambie ndugu zake Mungu akasema wanao Musa na manabii (Luka 16:29) Mungu huwa anasema ukitii utakula mema ya nchi maana yake usipotii hutakula mema hayo, pia neno la Mungu likowazi linasema mshahara wa dhambi ni mauti Mungu anajua wapi pa kupeleka mashambulizi za hiyo mauti anayoiongelea. Mungu hafundishwi na Mtu yeye anajua yote na anaweza yote.

Mungu ana kawaida ya kumwambia mtu kwa njia mbali mbali kama utakuwa mbishi kupitiliza atakuacha na akikuacha maana yake unakuwa halali ya shetani unakuwa chini ya laana bila kujijua. (Mithali 29:1), na atakuwa anajifariji kwa mahubiri ya shetani ambayo nayo ni injili nyingine inayompeleka mtu katika laana ya milele (Wagalatia1:8-9)

Watu wamekuwa wakifanya maovu mbali mbali kama kwamba Mungu amesinzia, amelala au haoni na sababu ya mambo kama hayo huweza kushusha ghadhabu ya Mungu kwa wanadamu na taifa na hata dunia yote, wakati mwingine Mungu husubiri labda huyu mtu atageuka pia huofia kupiga dunia pamoja na wema (Mwanzo 18:23-33) ingawa wakati mwingine huweza kuruhusu balaa Fulani limpate yeye aliye fanya tu. Ahimidiwe Mungu mwenye haki, amesema roho ya yeye atendaye dhambi ndiyo itakayo kufa, uzinzi mshahara wake ukimwi baadaye moto wa milele, mwizi mshahara wake kuchomwa moto baadaye adhabu ya milele, kuiba wake za watu mshahara wake kufumaniwa na kudhalilishwa, ingawa hapa kuna watu wengine huwasukumia kesi watu wengine mtu anaweza kufanya uovu fulani kwa kutumia cheo chake anaweza akabambikiwa kesi asiyehusika ili kumlinda mtu fulani, Mungu yote haya anayaona.

Ulimwengu huu tunaoishi una mwisho wake duniani hapa ni wapitaji tu hatuna muda mrefu wa kuishi sana sana unaweza kufikia labda miaka 60 au 80 au 100, baada ya kufa maisha yatakuwa ni milele umejiandaliaje umilele wako? Mwamini Yesu tembea naye kama akiba na kumtumikia kwa bidii, siku hizi maadui wa uhai wa mtu ni wengi mno karibu kila kitu hakina usalama hofu na mashaka vimeongezeka mno kuliko kawaida.Ajali nyingi siku hizi, magonjwa mengi,  vita visivyoisha duniani,uchawi tena una advance  kila kukicha, upo mpaka wa kununua, usalama wetu upo wapi?

Mkimbilie Yesu uwe salama uwe naye sasa ukimtumikia na kama utakufa kabla ya kuchukuliwa kwa kanisa utakuwa unaenda kula faida au matunda ya utumishi.(Wafilipi 1:21)

Watu wengine hudhani kuwa mtu anapokufa ndio safari imeishia hapo katika mwili huo ni  uongo wa shetani na mawakala wake, ndio maana watu wengine matatizo yanapowasibu asione pa kutokea huchukua uamuzi wa kipuuzi wa kujinyonga, ili apotelee mbali. Asikudanganye mtu yeyote ukifa ndio umeanza safari nyingine ya kuelekea nyumbani kwetu kwa milele ambako yatahusisha mwili wa roho mwili huu wa udongo tutauacha hapa duniani, maisha yako kuwa mazuri au mabaya itategemea uliishi vipi ulipokuwa hapa duniani, Muulize yule tajiri na masikini Lazaro, uone pia jinsi masikini alivyopewa heshima hata tu kwa kulitaja jina lake Lazaro, ila tajiri hakutajwa jina maana umaarufu wake ulikuwa huko duniani, na maisha yake yaliishia kikomo alitamani arudishwe tena duniani aanze moja ikashindikana kabisa, akamwomba Mungu atoke mtu kutoka kuzimu ashuhudie mateso, harafu akawaambie watu waishio duniani Mungu akasema hapana! Wanao Musa na manabii na wawasilize hao.(Luka mt 16:19-31).Hata hivyo kutokana na ombi la yule tajiri, kuna baadhi ya watu mbali mbali walishawahi kuchukuliwa na Yesu mwenyewe kwenda kuzimu na kurudi hapa duniani ili kushuhudia, japo kwa uchache mambo ya huko.

Pia kuna baadhi ya watumishi wa Mungu hufuatwa na kupewa kipawa cha kufanya miujiza ya kutisha ila ni nguvu kutoka upande ule wa adui wakipewa masharti wafanye miujiza lukuki ila si kuwahubiri watu habari za wokovu kuachana na zambi na huku wakiahidiwa kupewa mishiko (pesa) ya nguvu, na watu hao mawakala wa shetani, hapa sina maana miujiza yote inayofanyika kwenye nyumba za ibada inatoka kwa shetani ole kwa watumishi. Shetani hawapendi watu waliokombolewa. Sababu kuu ni kuwa wanafanya baadhi ya kazi zake zivurugike, maana wakati mwingine watu waliokombolewa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu huweza kugundua hila mbali mbali na makusudio yake aliyoipanga kwa wanadamu. Kama tujuavyo kuwa mipango mingi na mikakati mbali mbali ya shetani ilianzia kama maazimio katika vikao na kutoa maamuzi kwamba iwe hivi au vile, ili shetani atukuzwe. Ingawa watu wa Mungu nao kabla ya mikakati mbali mbali pia huanza kwa maazimio mbali mbali mfano:tufanye mkutano wa injili sehemu fulani ili watu wamgeukie Mungu wa kweli. Tukatembelee wagonjwa katika hospitali fulani

Mungu anawatafuta watu wanaotaka kumwabubu yeye katika roho na kweli kila siku, anza maisha mapya kwa kumkiri/ kumwamini Yesu/ kuongoka leo usisubiri kesho. (Mithali 27:1)

FANYA MAAMUZI BINAFSI YA KUMKUBARI YESU PEKEE KWA AJILI YA WOKOVU

Sali Sala ifuatayo kwa kumaanisha, tafuta mahali pa utulivu usali Mungu yupo kila mahali, (Yohana mt 4:24), hakuna mahali utakapokuwa Mungu asiwepo (Zaburi 139:7-8).

SALA:
“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”

Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.

1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku Warumi 10:17, Wakolosai 3:16

2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. Wathesalonike 5:17

3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa            linalokiri wokovu na kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. 1Petro         2:1-2, Waebrania 10:25.

4. Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione aibu, acha uvivu, tafuta pesa,              Mungu katoa  agizo tangu kale, Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo  hivyo  ( 2Thesalonike  3:10)

5. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani Ufu 3:11, Mwanzo 3:1-19 na 1Petro 5:8

6. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi                kujua  nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.Ufunuo 22:18 , Kolosai                4:16
                                             Ni mimi

Mtumishi Emmanuel T.M.Omari
injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com