(Matendo ya mitume 12:1- 19 Soma) Petro amefungwa minyororo chini ya ulinzi mkali
Katika
Jumuiya, ushirika aliokuwa akisali Petro, Yakobo na Roda (dada wa kazi) Kanisa
likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili ya Petro.
Kwa maombi
ya Wanajumuiya, Wanaushirika Petro anatolewa gerezani kiajabu na malaika wa
Mungu.
Anafika
jumuiya, ushirika aliokuwa akisali Petro akawakuta wenzake wanasali kwa bidii
ili Petro aachiwe.
Yakobo
alichinjwa kwa sababu kanisa wanajumuiya, washirika walikuwa hawaombi, hata kama
walikuwa wanaomba sio kwa mzigo.
Wakati mwingine tukipata changamoto ndo sisi binadamu tunaamka, wakati mwingine changamoto zinatuamsha.Pia Mungu anaweza ruhusu changamoto fulani au taabu ikupate ili usibweteke, (2Wakoritho 12: 7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.)embu waza u serious wa maombi kwa mtu anayeishi katika nchi yenye vita kila wakati kama Sudan na userious wa maombi kwa mtu anayeishi katika nchi yenye amani kama Tanzania.
Ulimwengu
wa roho upo na unafanya kazi na ndo una nguvu kuliko huu ulimwengu huu wa
mwili.
Ulimwengu
wa roho upo na una sehemu mbili kuna upande wa Mungu na upande wa shetani
Karibu
matukio yote yanayotupata au tunayopitia kawaida yanaanziaga rohoni kwanza
kabla ya kuonekana mwilini. Au kwa lugha nyingine kila tukio baya lililotokea katika ulimwengu wa mwili lilianzia ulimwengu wa roho wa Shetani na kila tukio zuri unaloliona limetokea katika ulimwengu wa mwili lilianzia ulimwengu wa roho upande wa Mungu.
Matukio mengi liwe jema au baya kabla ya kutokea mwilini Mungu anakuwa ameshayaona katika ulimwengu wa roho kwa neema yake ana uwezo wa kumfunulia mtu wake ili kuzuia madhara au kuruhusu jema kwa jamii husika Mungu anatizamaga mtu wake ili amshirikishe. Siri ya Bwana ipo kwao wamchao.
Katika kitabu cha Esta tunaona Esta akimwambia mjomba wake Mordekai kuwa wamuombee kwani anategemea kuenda kwa mfalme kinyume na taratibu ili kuokoa Wayahudi wasiuawe.( Est 4: 15-16 Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai, Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa kwa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa Mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.)
Katika Jumuiya, Ushirika alikokuwa akisali Petro, Yakobo na Roda Kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili ya Petro.
Pia Yesu
mwenyewe akiwa bustanini Gethemane alikuwa akiwaombea wanafunzi wake,ingawa
wanafunzi wake walikuwa wakikoroma hawamuombei, (Marko 14:41 Akaja mara ya tatu, akawaambia, Laleni
sasa mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama,Mwana wa Adamu anatiwa mikononi
mwao wenye dhambi. lakini pia Yesu ameenda mbinguni kwa Baba huko pamoja na
kutuandalia mahali, anatuombea pia.)
Musa baada
ya Wana wa Israeli kukosa, Mungu alikusudia kuwafutilia mbali Musa akaomba kwa
bidii kwa ajili ya wa wa Israeli Ili Mungu awasamehe uovu huu, Mungu akasikia
akasamehe uovu wao.
(Yakobo
5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa.
Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.)
Kwa kuwa
Mungu hawasikilizi wenye dhambi basi mwana wa Mungu embu changamka omba kwa
ajili ya wengine, pia kuna thawabu ukimuombea nabii kwa kuwa ni Nabii utapata
sehemu ya thawabu ya Nabii, kwa kuwa kila mtu duniani ana sehemu ya thawabu
katika uzima ujao ukifanya jambo jema kwa ajili yake haitakupotea thawabu yako
Mungu ni mwenye haki.
Mungu anaongea na
kila mtu kumjuza mambo ya mbele haijalishi ni mcha Mungu au la tatizo inaweza
kuwa tafsili, mfano wa mtu ambaye Mungu aliongea naye shida ikawa tafsili ni
pale Yusufu alipotiwa gerezani mnyweshaji wa mfalme an muokaji walivyoota ndoto
wakiwa gerezani, wakashindwa kuifasili ila Yusufu aliweza kuifasili (Mwanzo 40:1 – 13 Soma) pia kwa tukio hilo la Yusufu linatufundisha
kuwa wakati mwingine Mungu huongea na wengine kuhusu wewe kwa kujua au bila
kujua ili kupita katika changamoto fulani, ndo Mungu alivyo huwezi kuhoji sana
ndo Mungu utaratibu wake huo.
Wakati Yesu
amezaliwa kulikuwa na mtumishi wa Mungu ambaye Mungu alikuwa anamtumia kuandaa
mazingira mazuri ya Yesu kuzaliwa, huyu mtumishi alikuwa akiomba kwa bidii kwa
ajili ya Yesu, na Mungu alimtunza hakumuondoa duniani mpaka aje kushuhudia live
huyo mwokozi wa ulimwengu, na siku alivyozaliwa mtoto Yesu, Roho Mtakatifu alimuongoza huyu
mtumishi mpaka hekaruni akamuona Yesu, akashukuru na kusema sasa Bwana wamruhusu mtumishi wako aende kwa
amani kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu ... (Luka mt 2:29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, kwa
amani kama ulivyosema.)
Wakati Yesu anawaaga wanafunzi wake anaenda mbinguni aliwaambia kuwa anaenda kuwaandalia mahali, jambo jingine ni kuwaombea akiwa kule mbinguni, kwa hiyo kuombea wengine ni jukumu la kila mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo, na kuombea mtu mwingine ni bure, sio mpaka posho. Kama wanavyofanya manabii wa uongo wa siku hizi za mwisho, hata maandiko yana tushuhudia yakisema tumepewa bure, tutoe bure. Mungu ni wa wote wenye mwili matajiri kwa masikini.
Ushindi wa Joshua
Vitani ulitokana na maombi ya Musa pale mlimani
(Kutoka 17:8 – 15 Soma)
Pia sehemu nyingi
katika maandiko zaidi ya moja imeandika
mpende jirani yako kama nafsi yako (Mathayo
19:19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, mpende jirani yako kama nafsi
yako.)
Kabla ya Sodoma na
Gomora kuchomwa moto Mungu alikuwa akihojiana na Abrahamu, Abrahamu alikuwa
akiwakumbuka watu wa miji hiyo miwili mikubwa kwa kutaja idadi ya watu wenye
haki 50, 45,40,30,20 mpaka 10 kama idadi hiyo itakuwepo katika nchi bado Mungu
utahukumu? (Mwanzo 18:23 – 33 Soma)
Kwa kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi basi mwana wa Mungu embu changamka omba kwa ajili ya wengine, pia kuna thawabu ukimuombea nabii kwakuwa ni Nabii utapata sehemu ya thawabu ya Nabii, kwa kuwa kila mtu duniani ana sehemu ya thawabu katika uzima ujao ukifanya jambo jema kwa ajili yake haitakupotea thawabu yako Mungu ni mwenye haki.
Kuwakumbuka wengine
kuna Baraka zake sisi kama binadamu tuna tofautiana nguvu za mwili hata za
rohoni, tuwabebe wengine unaowajua na usiowajua Mungu mwenye haki
hatakuacha hivi hivi tu (Zaburi 40:1
Heri
amkumbukaye mnyonge; BWANA atamwokoa siku ya taabu.)
(Warumi 15:1 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na
nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.)
Sio hivyo tu hata
Mfalme suleimani baada ya kuchaguliwa awe Mfalme wa Israeli alitokewa na Mungu
katika ndoto, alivyoambiwa aombe chochote, alimwomba Mungu ' Kwa hio nipe mimi moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?" akapewa hekima Mungu
akambariki double double kwa kuwatanguliza wenzake kwa Mungu wake. (1 Wafalme 3:5 -14 Soma)
Paulo mtume katika makala zake karibu zote amekuwa akimaliza kwa kusema upendo wa Mungu Baba na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote, ni namna moja wapo ya kuombea kuwatakia mema wengine kama watu wa Mungu.
Kwa hiyo kama mkristo jifunze kuombea wengine mf.Yatima, wajane, wafungwa, wagonjwa sehemu mbali mbali hata kama huwajui au huna undugu nao huo nao ni utumishi wa Mungu unaonekana ni kitu kidogo machoni pa wanadamu ila kwa Mungu ni mkubwa sana, utumishi sio mpaka madhabahuni tu, pia tupo hapa duniani ili kumzalia Mungu matunda pamoja na kufanya kazi naye ukijizoeza kuombea wengine utajikuta Roho Mtakatifu akikuongoza kuombea mambo mbali mbali specific,na utabarikiwa na kuongezewa katika akiba yako ile iliyowekwa katika uzima wa milele.
Tusichoke kutenda mema, tusichoke kuombeana, sehemu nyingine maandiko yanatutia moyo kwa kusema tuombe bila kukoma. Ombea viongozi wa kiroho (Wachungaji, wainjilisti, mashemasi n.k) Ombea viongozi wa kimwili (Rais wa nchi, Mawaziri, wabunge, wajumbe, madiwani n.k) Kawaida Shetani akitaka kupiga kundi ana lenga hasa ampige kiongozi, sababu anajua nyuma ya watu hao kuna wengi, Imeandikwa (Mathayo 26:31 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga Mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.)
(I Wafalme 22: 31 – 33.
31 Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru wakuu wa magari yake thelathini na wawili, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake. 32 Ikawa wakuu wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Huyo ndiye mfalme wa Israeli Wakageuka juu yake ili wapigane naye; naye Yehoshafati akapiga ukelele. 33 Ikawa, wakuu wa magari walipoona ya kuwa siye mfalme wa Israeli, wakageuka nyuma wasimfuate.)
Kwa hiyo tujenge mazoea ya kuombea Nchi yetu, tutubu dhambi za watu wake na machafu nyote yanayotendeka kwa siri, sababu tusipoombea kiboko chake na sisi pia tunaweza kupata upepo upepo wake, mfano katika nchi kama hakuna mvua sababu ya kumwaga damu za watu wasio na hatia, wote tunaathirika. Mtumishi wa Mungu Danieli aliombea wengine na kupata majibu yake haraka sana, ingawa kikwazo kilikuwa ni mkuu wa uajemi, Mungu alituma malaika wakaenda kumpambania. (Danieli 9:5-23 Tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu na watu wote wa nchi ...)
Mimi nakushauri nikiwa kama mtumishi wa Mungu wa kawaida tu ukipata wasaa wa kuombea mfano watoto wako, mume wako, mke wako, babu au bibi yako usirundikie maombi watu walio wa damu yako zaidi kuliko walio damu mbali na wewe, ujue kuwa kuna watoto wengi, wake za watu na waume za watu wako magerezani wanahitaji maombi yako, ukiomba kwa kuegemea upande mmoja inawezekana kabisa ukakosa baadhi ya mambo hiyo ni kanuni za kiroho. Pia kumbuka kuwa maandiko yanatushauri, tuwapende jirani zetu kama nafsi zetu.
Mimi binafsi mara kadhaa Roho Mtakatifu amekuwa akinishuhudia niombee mambo mbali mbali ya watu wengine, wengine nawajua wengine siwajui unaweza kukuta Roho Mtakatifu anakuongoza kuombea mtu mwingine au tukio fulani la mbele tena kwa machozi, yaani picha inakujia unaona dhahiri bila chenga au unasikia kabisa unaambiwa ombea hiki, nami kama askari wa Bwana wajibu wangu ni kutii, jinsi Mungu alivyo wa ajabu.anawaambia watu wake kabla ya tukio husika kutokea, mambo kama haya sio rahisi kuelewa kwa mtu aliye nje ya Kristo hata humweleze vipi hataelewa ng'o. (Amos 3:7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.)
Ila pia katika maisha yangu binafsi mara nyingi najikuta huwa naombea zaidi watu wengine ndoa zao, kazi zao, watoto wao, uchumi wao, biashara zao kuliko hata kujiombea mwenyewe sijajua kwa nini ila nafanya kile ambacho nasikia kusukumwa kukifanya ndani yangu.
Sio hivyo tu bali kwa waumini walioamini na kupokea kipawa cha kunena kwa lugha, sababu ahadi hii ni kwa wote waaminio, unaweza kuomba kwa lugha mpya, Roho akikusukuma kutoa machozi, bubujika mwana wa Mungu, hapa hakika hujui unayoyasema ila ni lugha ambayo Shetani huwa anang'ang'aa macho hajui kinachozungumzwa, ni lugha ambayo unaongea na Mungu mwenyewe direct, ni neema iliyoje? Mungu atupe nini tena? Nikuulize swali hivi kama una uhitaji, shida fulani ya kumwambia Rais au Waziri ni kitu chepesi au utapata mlolongo wa taratibu ndeefu na vikwazo kibao ili kuongea naye, unaweza ambiwa tatizo lako nenda ofisi fulani watashughulikia, ila Mungu yeye anatualika sote twende kwake na habagui cha ajabu huyu Mungu tunaenda kwake moja kwa moja tunaomba kupitia jina la mwanwe mpendwa Yesu Kristo, tena maombi yenu yanakuwa ni siri baina yenu nyie wawili hasa pale unaponena kwa lugha, lugha hii hata malaika wanaambulia patupu ni wewe na Mungu tu, (1Wakorintho 14:2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake). fursa ipo kwetu sote. Tuchangamkie fursa.
No comments:
Post a Comment