Maisha yetu sisi binadamu tunaoishi chini ya jua yamejaa changamoto lukuki kila siku iitwayo leo, mpaka mahali Fulani wahenga waliwahi kusema ukiona kwako kunafuka moshi basi kwa jirani yako panateketea, kwa hiyo kila binadamu anachangamoto ya kwake, hamna mtu ambaye hana changamoto, hata mtu unayemuona leo anaishi kwa furaha, raha ya maisha au maisha kayapatia kuna muda furani katika maisha yake alipitia changamoto fulani, kwa hiyo tusinyongonyee na kujiona mnyonge sababu ya jambo lolote unalopitia maishani, hata mitume walipitia changamoto mbali mbali wengine walifia ndani ya changamoto. Hata Yesu mwana wa Mungu tena apendwaye, kuna kipindi alipitia katika changamoto, pia akasema duniani tunayo dhiki tujipe moyo. (Yohana mt.16:33 ” Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” )
Kwa hiyo kupitia changamoto katika maisha haina maana kuwa Mungu amekuacha au hakupendi, hakuoni au amekupotezea au unadhambi nyingi sana kuliko binadamu wengine, hapana kila changamoto ina sababu yake sio rahisi kuzitaja zote kwa sababu tumeumbwa tofauti tofauti, tuangalie baadhi ya watu waliopitia changamoto katika maandiko matakatifu:
YESU MWANA WA MUNGU
Yesu alidhalilishwa alipigwa,pigwa na mijeredi alichubuliwa , alivuliwa nguo, alivishwa taji ya miiba, akiwa ameshakata roho bado wakamuongezea na kumchoma mkuki ubavuni mwake.(Yohana 19:34 Lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji.)
ADAMU NA HAWA
Adamu na hawa waliingia mgogoro na Mungu mwenyezi, baada ya kutotii maagizo waliyopewa ya kutokula mti wa matunda ulio katikati ya bustani (Mwanzo 3: 9 – 24 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi ? Akasema, nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha …)
MUSA
(Hesabu 20 : 7-12 BWANA 7 akasema na Musa, akinena, 8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawotokezea maji katika mwamba hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao. 9 Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za BWANA kama alivyomwamuru. 10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mnbele ya mwamba, akawaambia, sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu? 11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia. 12 BWANA akamwambia Musa na Haruni, kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.)
YEREMIA
(Yeremia pamoja na kuambiwa kuwa yeye ni nabii wa mataifa lakini alipitia changamoto nyingi mno zilizohatarisha uhai wake kama sio Mungu kuwa karibu naye )
(Yeremia 36:5 -7 Yeremia akamwagiza Baruku, ya kwamba, Mimi nimefungwa, siwezi kuingia katika nyumba ya BWANA.Basi, enenda wewe, ukasome katika gombo la chuo, ambacho umeandika ndani yake, maneno ya BWANA yaliyotoka kinywani mwangu, ukiyasoma katika masikio ya watu, ndani ya nyumba ya BWANA, siku ya kufunga; pia utayasoma masikioni mwa watu wote wa Yuda watokao katika miji yao.Labda wataomba dua zao mbele za BWANA, na kurudi, kila mtu akiiacha njia yake mbaya; kwa maana hasira na ghadhabu ni kuu sana, alizotamka BWANA juu ya watu hawa. (Kifungoni)
(Yeremia 38: 4- 6 Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu,na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri , bali shari. Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lo lote kinyume chenu.Basi wakamtwaa Yeremia wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo. ( Shimo lililojaa matope)
ELIMELEKI
Naomi mama mjane aliye amua kukimbila ugenini ili asife kwa njaa, ameondoka mji wake akiwa na mumewe na watoto zake wawili wa kiume anarudi kutoka ugenini akiwa amefiwa na watoto wake na mumewe pia (Ruthu 1: 1 -5 1 Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi.Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. 2Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili ni Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. 3 Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na Yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. 4 Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili aliitwa Ruthu.Wakakaa huko yapata miaka kumi. 5 Wakafa na Maloni na Kilioni wote wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.)
DAUDI NA GOLIATH
(1 Samweli 17 : 45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.)
AYUBU
(Ayubu 2:3 BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ijapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.)
SAULI/PAULO
Sauli mkabaji na kuua watu mbali mbali wa Mungu na baadaye kuwa mtumishi mzuri wa Mungu aliye ongoza kwa kuandika nyaraka nyingi zenye mafundisho mbali mbali ya neon la Mungu. Akiwa katika ukabaji wake alikumbana na changamotop changamoto mbali mbali (Matendo ya mitume 9:1 -9 1 Lakini Sauli, akizidi kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, 2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3 Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski ; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi ? 5 Akasema, U nani wewe, Bwana ? Naye akasema, Mimi ndiye Yesu unayeniudhi wewe. 6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7 Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimnya, wakiisikia sauti wasioone mtu. 8 Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.) Na akiwa mtumishi wa Mungu pia alipata changamoto mara nyingi unaweza soma Matendo ya mitume 19:23 – 41 ( Utaona kuhubiri kwa Paulo kulipeleke Mji mzima wa Waefeso kuwa na ghasia na kuhatarisha uhai wa Paulo) na Matendo ya mitume 23:12 – 24 (Njama za watu 40 kutokula mpaka watakapomuua Paulo na Askari 470 kupangwa ili kuvunja huo mpango). Pia Paulo ni mtume ambaye alikaa muda mrefu vifungoni pia ilipelekea kuandika nyaraka nyingi zinazofundisha misingi ya ukristo.
WANAFUNZI WA YESU
Nawaelezea baadhi Thomaso huyu aliuwawa kwa kupigwa na mshare India ya sasa. Petro aliuwawa kwa kusurubiwa kama Yesu ila msaraba wake uligeuzwa kinyume na ule wa Yesu. Mathayo aliuwawa kwa upanga baada ya kuonyesha msimamo katika imani ya Kikristo. Yohana huyu alitumbukizwa katika pipa linalochemka la mafuta lakini kwa miujiza ya Mungu hakuungua huko Roma Italia ya sasa.Mwishoni wakampeleka katika gereza lililokuwa migodini katika kisiwa Patmos, ambako huko alitokewa na Yesu akaandika kitabu cha ufunuo.Luka alinyongwa huko ugiriki kutokana na msimamo wake hadi akafa.
Sio rahisi kuziorodhesha changamoto zote walizopitia watumishi mbali mbali wa Mungu, kuna vitu wamefanyiwa watumishi wa Mungu ambavyo havikurekodiwa ilikuwa sio rahisi kwa waandishi wa biblia kurekodi kila kitu tunachosoma leo au kusikia, ni baadhi ya mambo tu yamerekodiwa ingekuwa kurekodiwa kila kitu biblia ingekuwa ni kitabu kisichobebeka kwa ukubwa.(Yohana mt 21:25 Kuna mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.)
Sala ya kuombea marehemu
Kuna watu wanavurunda wakiamini kuwa kwa kuwa wana mahusiano mazuri na watumishi fulani fulani wa Mungu basi siku wakifa watasaliwa sala ndefuuu au kumwagiwa maji ya baraka au mafuta ya upako itakayopelekea Mungu kubadilisha maamuzi ya badala ya kuwapeleka motoni waende mbinguni, ndugu yangu usidanganyike chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna, Pia Mungu hana kigeugeu, roho itendayo dhambi itakufa. Sala zetu za kuombea marehemu hazina kitu kabisa ni utaratibu tu wa kujaribu kufariji wafiwa wasifikie, wasiamue maamuzi yatakayopelekea kuongeza matatizo juu ya matatizo. Kama umekorofishana na Muumba ni nani Malaika yupi, Askofu gani, Mtume na nabii gani atakayeweza ingilia kati arudishe mahusiano kama sio Yesu pekee, unayetakiwa kutengeneza mahusiano naye wakati ukiwa hai? Kuna makosa wanayofanya baadhi ya watumishi Maaskofu, Wachungaji na manabii ya Kususia kutoenda kufanya ibada ya mazishi kwa sababu aliyekufa amejinyonga ni laana, lakini kuna watu wamekuja kushiriki mazishi hayo wanahitaji injili ili wamgeukie Mungu, unajuaje kuwa hiyo ni fursa kwake ya kuipata injili ya mwokozi, acheni hizo zenu kujifanya watakatifu sana? siku hizi binadamu tumebadilika, yameshawahi kutokea watu wanamuua mtu afu wanaweka mazingira fulani ionekane kama amejinyonga lakini ki uhalisia sio kweli, ni mchezo tu amefanyiwa marehemu siku hizi wanauwa wengine kisomi.Wanaweza kuuchunguza mwili pia wanaweza wasitambue ukweli ni upi.
Maisha yetu tunayoishi kila siku
Na ni kawaida kwa maisha tunayoishi hapa duniani kuona, kusikia changamoto mbali mbali wanazopitia watu mbali mbali nani ukweli usiopingika kuwa ukiona wewe unachangamoto furani basi ujue kuna mwenzako anapitia changamoto, shida kama yako au zaidi ya hiyo kwa unayopitia. Tena ukitaka kujua, kuona tembelea mahospitalini uone watu wanavyopitia shida, magonjwa, changamoto mbali mbali.Na changamoto hizo hazichagui mtoto, kijana, mzee.
Baadhi ya changamoto zinazopelekea watu kujiua, kujinyonga, kwa nchi mbali mbali
- Mambo ya mapenzi. (Fumanizi, ujauzito kukataliwa, kukataliwa na mpenzi wa kike au kiume, kubakwa, lawitiwa,kiungo fulani cha mwili kutofanya kazi ipasayo, kutalikiana, kusalitiwa )
- Maradhi sugu (Pumu, kisukari, Ukimwi, ugonjwa wa akili, kansa, kifafa).
- Wenza kufumaniana na kugundua kuwa mwezi mmoja kiume ana tabia za ushoga au kufumwa kwa mwenza wa kike kuwa na tabia ya usagaji ambayo haikujulikana hapo kabla.
- Ulevi kupindukia na matumizi ya madawa haramu ya kulevya
- Maisha (Kufukuzwa kazi, msongo wa mawazo, kufeli mtihani, madeni sugu na kuyumba kiuchumi, kukata tamaa,kusemwa na kusimangwa)
- Kusikia sauti za watu wasionekana kwa macho ya nyama wakimshawishi muhusika ajiue, kuumbuliwa kwa jamaa wa karibu katika uchawi.
- Kurithi, historia ya mambo kama hayo kwa baadhi ya familia.
- Kifungo cha miaka mingi kwa mwenzi mmoja wa kike au kiume.
- Kuna watu wanaua watu wengine afu wanawaninginiza ili watu wakija kuangalia waseme wamejinyonga, hao waliofanya jambo hilo la kinyama hawajaonwa na mtu lakini wameonwa na mmoja aonaye kila mahali ni Mungu na hawezi kuwaacha hivi hivi watapata mshahara wake ambao ni mauti ya milele.
- Wengine wanapiga risasi wengine na wao kujiua, jambo ambalo hata shetani mwenyewe hawezi kulifanya, kama shetani angeweza kufanya basi leo hii tusingekuwa na shetani na malaika na mapepo wake, vibwengo na majini na vinyamkera.
- Je huna dini wewe? kwa nini usiwaone viongozi wako wa dini ili wakuombee, au nenda kwa wazazi au walezi , marafiki wa karibu unaowaamini? Watakutunzia siri? Marafiki ni watu tulionao karibu tunaoshirikiana nao katika shida na raha, pia ni muhimu katika maisha kuwa na rafiki unayemuamini, kushare changamoto na mwenzako ni njia moja wapo ya kuutua mzigo lakini pia maandiko yanasema tumtwishe Yesu Fadhaa zetu, je umemshirikisha amekujibuje? (1Petro 5:7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.)
- Ukijiua ni sawa sawa kabisa na kuua umemtenda Mungu dhambi na unastahili adhabu, kiboko cha Mungu. Maandiko yanasema mshahara wa dhambi ni mauti, tena mauti ya milele. (Warumi 6: 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.)
- Kila shida iliyopo duniani wewe sio wa kwanza kuna wengine wanashida zaidi ya yako mara tatu mpaka nne zaidi, hawajakata tamaa na wanaishi duniani, lakini pia mafanikio mengine hayaji kirahisi rahisi mpaka upitie changamoto fulani.
- Kila mtu yupo duniani yupo kwa kusudi fulani la kiMungu, yeye ndio ameruhusu uje duniani na yeye ndiye atakaye ridhia wewe uondoke katika dunia hii baada ya kuona kusudi lake alilolipanga limekamilika. (Yohana mt 15:1-2 1mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.2Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.)
- Kuna baadhi ya watu wapo duniani tena wengine ni ndugu wa karibu au mzazi au mtoto wana wachawia wenzao wanawatesa wenzao kwa kuwapatia ugonjwa wa akiri, magonjwa yasiyo tibika, au mlogwaji kujichukulia uamuzi wa kujiua ili mlogaji apate utajiri wa chap chap ila Mungu anajua kila kitu utakuja toa hesabu. Kuna nyumba kijana wao wa kwanza ni wa kitandani muda wote, siku moja mama mzazi wa huyu kijana mgonjwa aliniita nikamwone, baada ya kwenda kumuona da ni huruma kwa kweli huwezi amini , Nilitaka kufanya huduma nikasikia sauti inaniambia "baba mtu anahusika na mchezo mchafu huu" hapo hapo nikaanza kuona vikwazo toka kwa mzazi wa kiume, sikuendelea na maombi nikajiondokea kimya kimnya sikurudi. Sijaonana na mama mtu siku nikimwona nitamwambia aende kanisa la jirani.
- Nyumba za ibada zikiwa chache kuliko nyumba za starehe bar, Casino, Vijumba vya waganga wa kienyeji ni rahisi matukio ya kujiua kuongezeka katika jamii husika.
- Utandawazi wa siku hizi wa kuwapa uhuru uliopitiliza watoto wetu tuliowazaa wa kuangalia internet au chochote kinacho oneshwa katika internet na Tv, sio kitu kizuri kwa watoto, sio hivyo tu bali siku hizi kuna moves nyingi nyingi baadhi sio nzuri kwa watoto unaweza kukuta kuna moves watu wanapigana bastola, visu, mishale baadhi ya vitu watoto wakitazama kwa muda mrefu inaweza kuwaathiri na kujikuta wakitaka kufanyia zoezi kile kitu walichokiona luningani au kwenye internet. Kuna moves fulani fulani origin yake ni kwa mawakala wa shetani wamepanga kupenyeza vitu fulani fulani kwenye jamii yetu kwa siri.
- Binadamu wote siku moja tutakufa, na kila mtu akifa ana takiwa kutoa ripoti yake mbele za Mungu, wewe uliyejinyonga utatoa taarifa gani? (Warumi 14: 12 Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.)
Katika utafiti uliofanywa na shirika la afya ulimwenguni (WHO) na matokeo yake kutangazwa kuwa taarifa rasmi ya umoja wa mataifa (UN) Mwaka 2014 inaeleza kuwa katika kila sekunde 40 mtu mmoja duniani hujiua. Pia kila Septemba 10, ni siku ya kimataifa ya kuzuia kujiua ambapo amasisho za kuzuia kujiua zinatolewa kote duniani.
Kabla ya kujiua tafakari yafuatayo kwa umakini
Hata watu unaowaona wanaishi kwa raha leo ujue ya kuwa kuna kipindi katika maisha yao walipitia mateso furani, kwa hiyo taabu au mapito ni ya muda na Mungu yupo pamoja na wewe sio kwa sababu hakupendi. lakini ujue ya kuwa wakati mwingine Mungu huruhusu taabu. mateso na changamoto upitie ili baadaye aje kuwaaibisha waliokucheka na kukudharau kwa hiyo ndugu usife moyo.
Kwa nini ifike mahali Mungu ajute kwa kutuumba, akasirike kwa ajili yetu sisi binadamu na kughairi kuwa alituumba, kwa nini tumsumbue Mungu muumbaji? Mungu ambaye ambaye hapendi kelele.
Mtu aliye kwenye mateso makali kuliko wote
Kwenye biblia kuna mtu ametajwa aliye kwenye mateso makali yasiyo elezeka ni kulia tu muda wote, huyu ndio angetakiwa atamani kujiua ingeeleweka, lakini hatamki swala la kujiua iweje wewe duniani utamani kujiua? Embu msome afu mlinganishe mateso yake na yako unayopitia
(Luk 16: 19 – 31 19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya Yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa Yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa akazikwa.23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sis na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. 31 Akamwambia, wasipowasikia Musa na Manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.)
Mtu huyo yupo kwenye mateso ya moto usiozimika na kiu ya ajabu ya kutamani kuburudishwa japo na tone la maji bila kulipata. Iweje leo wewe mtu unaye ishi duniani na kufurahi katika dunia yenye uwepo wa Mungu, ulinzi wake, wema wake, upendo wake wa kutufia msarabani, neema yake, furaha yake, roho wake na mema yake mengi mengi kila iitwapo leo. Mungu anatutendea mema mengi kila siku, iweje leo Mungu kuruhusu baya moja tu kwako likupitie ulalamike sana hata upelekee kukufuru? Ya kutaka kujiiua au kujizuru?
(Ayubu 2:10 10 Lakini yeye akamwambia, wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya ? katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.)
Sisi kama binadamu sio sawa kumlalamikia Mungu na Badala yake ni kushukuru kwa kila jambo linalotendeka, kwa sababu katika kila jambo Mungu ana makusudi yake ambayo ni yeye Mungu anayejua peke yake.Pia katika kila pito au changamoto mtu anayopitia ujue kuna mtu anapitia changamoto nzito zaidi duniani hapa, Yeye kama mfanyanzi na sisi ni udongo tumwache Mungu afanye mapenzi yake.
Tamati namalizia kwa kusema ili kuondokana na nia ovu ya kujiua/ Kujinyonga Omba Toba mbele za Mungu akusamehe nia yako ovu hiyo, Mungu ni mwaminifu yupo kila pahali atakusaidia, lakini pia ukishindwa mwite mtu unayemuamini akusaidie katika tatizo, shida hiyo, Bila shaka Mungu atafanya njia au mlango wa kutokea na kushinda hilo jaribu,(1 Kor 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi,isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kushahimili). nawe utaishi kwa furaha na amani kama wengine, Ubarikiwe na Bwana Yesu.
Kama utakuwa tayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.
“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”
Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.
1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku. (Warumi 10:17), (Wakolosai 3:16)
2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike 5:17)
3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri wokovu na kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25)
4. Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione aibu, acha uvivu, tafuta pesa, Mungu katoa agizo tangu kale, Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo hivyo, (2Thesalonike 3:10)
5. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani. (Ufunuo 3:11), ( Mwanzo 3:1-19) (1Petro 5:8)
6. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) ,( Kolosai 4:16)
Ni mimi
Mtumishi Emmanuel T.M.Omari
injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com