Tuesday, August 30, 2022

MLANGO WA MBINGUNI

 






Mlango ni njia ya kuingia mahali na kutokea

Katika miji kawaida kuna kuwa na milango ya miji kwa ajili ya usalama wa mji husika, hata katika Israeli kulikuwa na ukuta na inasemekana kuna milango 12, na Bwana Yesu katika utumishi wake hapa duniani alikuwa na mitume 12, pamoja na mmoja kukengeuka akamweka mwingine aliye chukua nafasi ya Yuda Iskariote anayeitwa Mathiya.

Dini au Madhehebu ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu na Wokovu ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu.

Dhambi ya Adamu na Hawa ilipelekea dunia yote kuwa chini ya Shetani na shetani akawa ndio  mungu wa dunia hii, (2Wakorintho 4:4 Ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasio amini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.) mungu si ndio anayeamua nini kifanyike katika dunia, Shetani huamua ajari itokee, maafa yatokee na kweli huwa  yanatokea. Wakati mwingine neema huweza tokea yakazuiwa katika maombi siri hii wanayo baadhi ya walokole ambao wanadharaulika katika jamii wanaonekana kama wamechanganyikiwa au hawana elimu, au pesa. si kila mtu aliyeokoka anaweza badilisha tukio wengine ni walokole feki, kwa hiyo tukio baya linageuzwa na kuwa jambo jema na Mungu anajipatia utukufu (Yeremia 1:10 angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa na kuharibu na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.) maana shetani hutuwazia mabaya kila siku na yeye kazi yake ni kuua kuharibu. (Yohana Mtakatifu 10:10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu ; mimi nalikuja ili wawe na uzima , kisha wawe nao tele.)

Leo hii kuna dini lukuki wengine wanasali Jpili, Jmosi,Jtatu kila mmoja anadai siku yake ndio sahihi, wengine wanaabudu na kujitumainisha kuwa siku wakifa watamiliki majengo na magari na kuishi kama paradiso, hapa hapa duniani wengine wanamuabudu mama na kudharau mtoto, wanakuambia mtoto na mama bora mama, mtoto Yesu hana kitu Makanisa ya mashetani yapo wazi wala siku hizi sio kificho na wanatafuta waumini kwa bidii kweli, Mbeya kuna kuna kanisa wanaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja na kunywa pombe tani yako na wana maandiko ya kusimamia, kuoa mke zaidi ya mmoja ruksa Mbona Yakobo alioa au Daudi, Yakobo walioa kwa hiyo ruksa. Ukifuatilia madhehebu ni mkorogano mtupu unaweza kuchanganyikiwa twende kanisa gani lipo sahihi maana kila kanisa linadai lenyewe ndio sahihi kuliko lingine, kuna siku nilienda kanisa la Nabii mmoja anafanya miujiza miujiza akawa ana jock makanisa mengine anasema njoo huku umwone mungu live achana na makanisa mengine ambako mungu wao amelala.

(Yoh 10: 9 Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.) Yesu anasema yeye ndiye mlango hivyo akili zetu zinajua mlango wa kuingia mahali na kutoka katika uumbaji mlango hauna maana ya kitu bali mtu ndio maana Yesu anasema  ‘mimi ni mlango’ haina maana tunafungua mdomo au kinywa chake tunaingia tumboni mwake , ni mtu anayeweza kufanya jambo fulani na kusababisha jambo kutokea.

(Mathayo 16:18 Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda, milango ya kuzimu ni mapepo)

Kama vile ambavyo mtu anakuwa na ratiba zake kwa siku au kwa mwaka naye Mungu ana ratiba zake ni kweli lango lipo wazi kuna muda hili lango litafungwa halitafunguliwa ngo.

Kuna wimbo wa Kikristo unasema LIPO LANGO MOJA WAZI NI LANGO LA MBINGUNI

(Luka mt 9:23 – 24 Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe ajitwike msaraba wake kila siku, na anifuate.Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza , na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.)

Ndo maana hata wanafunzi wa Yesu karibu wote vifo vyao vilikuwa ni vya mateso sana ili kusudi wakate tamaa waachane na Yesu wapotee milele, Petro alisurubiwa katika msaraba uliogeuzwa kinyume na ule wa Yesu, Yohana alitupwa kwenye pipa la lami inayochemka akawa hafi mwishowe wakamtupa kwenye kisiwa cha patmos, huko akaja kuandika kitabu cha ufunuo, Tomaso alipigwa mshale alipokuwa ameenda katika shughuli za kimisionari huko India, Paulo ni mtume aliyefungwa muda mrefu gerezani pia huko akawa akiandika nyaraka vitabu mbali mbali baadaye alichinjwa. Stefano alipigwa kwa mawe hadi akafa. Kwa hiyo ugumu wa njia hii walioupitia wenzetu ndo nasi tunapitia ukitaka mteremko basi safari yako mwisho wake ni mbaya. Utachukiwa na dunia na shetani pia (Luka mt 10:23 “Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka”)

Pia mtumishi Adam haji Aliyeokokea Somalia ameshuhudia mahali alipoamua kumuoa msichana mmoja na huyo msichana alipoamua kuokoka aliingizwa kisu katika uke wake na kuinuliwa juu na kupasuliwa katikati na kufa hapo hapo.

Yesu ametoa tahadhali njia ya mbinguni sio lele mama ina vita vikali, Shetani anapambana na wote ili kuwakatisha tamaa waishie njiani warudi nyuma ili wakosee nao waingie mlango wa kuzimu alioandaliwa Shetani na Malaika zake mwanadamu ataingia huku kwa kutojari au kutowasikiza akina Musa na manabii kama tahadhari, kama yule tajiri aliyeingia motoni na kutamani kurudi duniani japo dakika moja haikuwezekana.

Yule bwana mjinga likwenda bila cheti, Mbinguni watu hawaingii kiholela holela tu kuna utaratibu ndo maana utakuta sehemu nyingine katika mifano ya Bwana Yesu ametumia kama siku ya harusi ya mwanakondoo, yaani kuingia hapo ni kwa watu maalumu wenye cheti yaani Wokovu bila hicho njia nyeupe nenda kuleeee mbali motoni kilio na kusaga meno milele.

(Zaburi 118: 20 Lango hili ni la BWANA, Wenye haki ndio wataoliingia.)

Haki tunaipata baada ya kumkiri Kristo Mwana wa Mungu aliye hai pekee, usipomkiri, ukikata basi ujue hukumu inakusubiri na moto wa jehanamu unao tamani upate chakula chake, yaani watu wasiomkiri Yesu katika kipindi hiki cha neema kabla lango halijafungwa, likifungwa halitafunguliwa ng'o milele.

Ukikosa sifa za kuingia katika lango la mbinguni basi wewe utakuwa na sifa za kuingia katika mlango wa kuzimu utapokelewa na wenyeji wa huko kwa ajili ya mateso ya milele pamoja na shetani, tuamue leo watu wengi hawajamkiri Kristo wanajifariji kuwa wataingia mbinguni kwa sababu wanaimba kwaya au wanatumika madhabahuni, wamepata komunio, kipaimara, mbinguni watu unaingia kwa kumkiri Yesu kwa kinywa chako mwenyewe (Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa ni Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.) Kumwamini Yesu ni hiyari hakuna anayelazimishwa kuamua hivyo kwa sababu karibu mambo mengi ya Mungu tunatakiwa tufanye kwa hiyari kwa moyo wa kupenda bila kulazimishwa, ila ndo hivyo ukikubari utakula mema ya nchi ukikataa basi hukumu inakusubiri.

Kutokubali kumkiri Yesu ni kutokubariana na Mungu uamuzi wake wa kumtoa Yesu afe msarabani na kutulipia deni na badala yake unakuwa upo tayari kulilipa mwenyewe bila msaada wa Mungu, na ili kulilipa hili deni ni kuingia katika moto wa milele pamoja na Shetani yaani tunakuwa tunaona kama vile Shetani ameonewa bora twende motoni wote, ingawa ule moto Mungu aliuandaa kwa ajili ya Shetani na malaika zake.(Mathayo mt 25:41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na  malaika zake.) Binadamu ataingia kwa kujitakia mwenyewe. Kwa sababu binadamu yeyote aliye hai Duniani leo ana maamuzi ya kuchagua kwa hiyari yake mwenyewe njia aitakayo aende motoni au mbinguni? baada ya kufa hakuna nafasi hiyo tena. Kama yupo mtu yeyote anatumainia baba au babu ni kiongozi mkubwa sana wa dini akuombee sala nzito ya kuwekwa mahali pema peponi ni uongo wa mchana kweupeee. Mungu hana kigeu geu (Malaki 3:6  Kwa kuwa mimi; BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo) 

Pia kama utatangulia mbele ya haki ndo neema yako itakuwa imeishia hapo, sababu maandiko yanasema baada ya kifo kinachofuata ni hukumu. (Waebrania 9: 27 – 28 27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtamiao kwa wokovu.)

Kuna watu wengi wataingia motoni kwa kudhani  kuwa baba au mama walikuwa ni Wakristo basi automatic na wao ni wakristo hivyo mlango wa mbinguni ni halali yao haipo hivo dini sio kabila.Mahusiano ya mtu au binadamu na Mungu wake ni ya binafsi mtu na Mungu wake sio kufuata mkumbo, kurithi. Na kila mtu atasimama mbele za Mungu kueleza habari zake (Warumi 14:12 Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.) Wengine katika kanisa huenda wanafanya huduma za madhabahuni mf. Uzee wa kanisa , Ushemasi, kuongoza sifa, Kuomba na hata kutoa mapepo hivyo vyote sio tiketi ya kuingia Mbinguni, Mbinguni tunaingia kwa tiketi moja tu ya wokovu, unao patikana kwa Yesu pekee sio mtu yeyote Maria, Petro, Muhamedi, Zumaridi, Paulo au mtume yeyote aliyepo au atakayekuja na kufanya miujiza kabambe. (Matendo ya mitume 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.)

Mungu hana upendeleo anatupenda binadamu wote na pia anatuwazia mema, ila hapo hapo Shetani hatuwazii mema anatamani watu wote duniani tuikose mbingu, twende motoni pamoja naye kwa hiyo binadamu tunatakiwa tujiongeze, tujue lengo la Mungu na lengo la Shetani na kufanya uamuzi wa kuchagua,Yoshua 24: 15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakaye mtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. (2 Wakorintho 6:2 Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia ; tazama, Wakati ulikoubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndio sasa.) Tuchague leo, sio kesho, hatujui kesho yako, Amina Barikiwa.

Kama utakuwa tayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.


“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”


Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.

1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku. (Warumi 10:17), (Wakolosai 3:16)

2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike   5:17)

3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri  wokovu na      kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25)

4.  Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione aibu, acha uvivu, tafuta pesa, Mungu katoa                         agizo tangu kale, Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo hivyo,   (2Thesalonike                       3:10)

5. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani. (Ufunuo 3:11), ( Mwanzo 3:1-19) (1Petro 5:8)

6. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) ,( Kolosai 4:16)


                                                                               Ni mimi 

Mtumishi Emmanuel T.M.Omari
injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com




 

Ah !!! Bora nife, nijiue NIKAPUMZIKE, niondokane na hizi changamoto zisizoisha kila siku shida haziishi, BORA HATA NISINGEZALIWA.




Maisha yetu sisi binadamu tunaoishi chini ya jua yamejaa changamoto lukuki kila siku iitwayo leo, mpaka mahali Fulani wahenga waliwahi kusema ukiona kwako kunafuka moshi basi kwa jirani yako panateketea, kwa hiyo kila binadamu anachangamoto ya kwake, hamna mtu ambaye hana changamoto, hata mtu unayemuona leo anaishi kwa furaha, raha ya maisha au maisha kayapatia kuna muda furani katika maisha yake alipitia changamoto fulani, kwa hiyo tusinyongonyee na kujiona mnyonge sababu ya jambo lolote unalopitia maishani, hata mitume walipitia changamoto mbali mbali wengine walifia ndani ya changamoto. Hata Yesu mwana wa Mungu tena apendwaye, kuna kipindi alipitia katika changamoto, pia akasema duniani tunayo dhiki tujipe moyo. (Yohana mt.16:33Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu” )

Kwa hiyo kupitia  changamoto katika maisha haina maana kuwa Mungu amekuacha au hakupendi, hakuoni au amekupotezea au unadhambi nyingi sana kuliko binadamu wengine, hapana kila changamoto ina sababu yake  sio rahisi kuzitaja zote kwa sababu tumeumbwa tofauti tofauti, tuangalie baadhi ya watu waliopitia changamoto katika maandiko matakatifu:

YESU MWANA WA MUNGU

Yesu alidhalilishwa alipigwa,pigwa na mijeredi alichubuliwa , alivuliwa nguo, alivishwa taji ya miiba, akiwa ameshakata roho bado wakamuongezea na kumchoma mkuki ubavuni mwake.(Yohana 19:34 Lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji.) 

ADAMU NA HAWA

Adamu na hawa waliingia mgogoro na Mungu mwenyezi, baada ya kutotii maagizo waliyopewa ya kutokula mti wa matunda ulio katikati ya bustani (Mwanzo 3: 9 – 24 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi ? Akasema, nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha …)

MUSA

(Hesabu 20 : 7-12 BWANA 7 akasema na Musa, akinena, 8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawotokezea maji katika mwamba hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao. 9 Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za BWANA kama alivyomwamuru. 10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mnbele ya mwamba, akawaambia, sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu? 11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia. 12 BWANA akamwambia Musa na Haruni, kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.)


YEREMIA

(Yeremia pamoja na kuambiwa kuwa yeye ni nabii wa mataifa lakini alipitia changamoto nyingi mno zilizohatarisha uhai wake kama sio Mungu kuwa karibu naye )

(Yeremia 36:5 -7 Yeremia akamwagiza Baruku, ya kwamba, Mimi nimefungwa, siwezi kuingia katika nyumba ya BWANA.Basi, enenda wewe, ukasome katika gombo la chuo, ambacho umeandika ndani yake, maneno ya BWANA yaliyotoka kinywani mwangu, ukiyasoma katika masikio ya watu, ndani ya nyumba ya BWANA, siku ya kufunga; pia utayasoma masikioni mwa watu wote wa Yuda watokao katika miji yao.Labda wataomba dua zao mbele za BWANA, na kurudi, kila mtu akiiacha njia yake mbaya; kwa maana hasira na ghadhabu ni kuu sana, alizotamka BWANA juu ya watu hawa. (Kifungoni)

(Yeremia 38: 4- 6 Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu,na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri , bali shari. Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lo lote kinyume chenu.Basi wakamtwaa Yeremia wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo. ( Shimo lililojaa matope)

ELIMELEKI

Naomi mama mjane aliye amua kukimbila ugenini ili asife kwa njaa, ameondoka mji wake akiwa na mumewe na watoto zake wawili wa kiume anarudi kutoka ugenini akiwa amefiwa na watoto wake na mumewe pia (Ruthu 1: 1 -5 1 Ikawa zamani za Waamuzi walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi.Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. 2Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki, na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili ni Maloni na Kilioni, Waefrathi wa Bethlehemu ya Yuda wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. 3 Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na Yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. 4 Nao wakaoa wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili aliitwa Ruthu.Wakakaa huko yapata miaka kumi. 5 Wakafa na Maloni na Kilioni wote wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.)

DAUDI NA GOLIATH

(1 Samweli 17 : 45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.)

AYUBU

(Ayubu 2:3 BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ijapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.)

 

SAULI/PAULO

Sauli mkabaji na kuua watu mbali mbali wa Mungu na baadaye kuwa mtumishi mzuri wa Mungu aliye ongoza kwa kuandika nyaraka nyingi zenye mafundisho mbali mbali ya neon la Mungu. Akiwa katika ukabaji wake alikumbana na changamotop changamoto mbali mbali (Matendo ya mitume 9:1 -9 1 Lakini Sauli, akizidi kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, 2 akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3 Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski ; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi ? 5 Akasema, U nani wewe, Bwana ? Naye akasema, Mimi ndiye Yesu unayeniudhi wewe. 6 Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7 Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimnya, wakiisikia sauti wasioone mtu. 8 Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.) Na akiwa mtumishi wa Mungu pia alipata changamoto mara nyingi unaweza soma Matendo ya mitume 19:23 – 41 ( Utaona kuhubiri kwa Paulo kulipeleke Mji mzima wa Waefeso kuwa na ghasia na kuhatarisha uhai wa Paulo) na Matendo ya mitume 23:12 – 24 (Njama za watu 40 kutokula mpaka watakapomuua Paulo na Askari 470 kupangwa ili kuvunja huo mpango). Pia Paulo ni mtume ambaye alikaa muda mrefu vifungoni pia ilipelekea kuandika nyaraka nyingi zinazofundisha misingi ya ukristo.

 

WANAFUNZI WA YESU

Nawaelezea baadhi Thomaso huyu aliuwawa kwa kupigwa na mshare India ya sasa. Petro aliuwawa kwa kusurubiwa kama Yesu ila msaraba wake uligeuzwa kinyume na ule wa Yesu. Mathayo aliuwawa kwa upanga baada ya kuonyesha msimamo katika imani ya Kikristo. Yohana huyu alitumbukizwa katika pipa linalochemka la mafuta lakini kwa miujiza ya Mungu hakuungua huko Roma Italia ya sasa.Mwishoni wakampeleka katika gereza lililokuwa migodini katika kisiwa Patmos, ambako huko alitokewa na Yesu akaandika kitabu cha ufunuo.Luka alinyongwa huko ugiriki kutokana na msimamo wake hadi akafa.

 

Sio rahisi kuziorodhesha  changamoto zote walizopitia watumishi mbali mbali wa Mungu, kuna vitu wamefanyiwa watumishi wa Mungu ambavyo havikurekodiwa ilikuwa sio rahisi kwa waandishi wa biblia kurekodi kila kitu tunachosoma leo au kusikia, ni baadhi ya mambo tu yamerekodiwa ingekuwa kurekodiwa kila kitu biblia ingekuwa ni kitabu kisichobebeka kwa ukubwa.(Yohana mt 21:25 Kuna mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.)

Sala ya kuombea marehemu

Kuna watu wanavurunda wakiamini kuwa kwa kuwa wana mahusiano mazuri na watumishi fulani  fulani wa Mungu basi siku wakifa watasaliwa sala ndefuuu au kumwagiwa maji ya baraka au mafuta ya upako   itakayopelekea Mungu kubadilisha maamuzi ya badala ya kuwapeleka motoni waende mbinguni, ndugu yangu usidanganyike chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna, Pia Mungu hana kigeugeu, roho itendayo dhambi itakufa. Sala zetu za kuombea marehemu hazina kitu kabisa ni utaratibu tu wa kujaribu kufariji wafiwa wasifikie, wasiamue maamuzi yatakayopelekea kuongeza matatizo juu ya matatizo. Kama umekorofishana na Muumba ni nani Malaika yupi, Askofu gani, Mtume na nabii gani atakayeweza ingilia kati arudishe mahusiano kama sio Yesu pekee, unayetakiwa kutengeneza mahusiano naye wakati ukiwa hai? Kuna makosa wanayofanya baadhi ya watumishi Maaskofu, Wachungaji na manabii ya Kususia  kutoenda kufanya ibada ya mazishi kwa sababu aliyekufa amejinyonga ni laana, lakini kuna watu wamekuja kushiriki mazishi hayo wanahitaji injili ili wamgeukie Mungu, unajuaje kuwa hiyo ni fursa kwake ya kuipata injili ya mwokozi, acheni hizo zenu kujifanya watakatifu sana? siku hizi binadamu tumebadilika, yameshawahi kutokea watu wanamuua mtu afu wanaweka mazingira fulani ionekane kama amejinyonga lakini ki uhalisia sio kweli, ni mchezo tu amefanyiwa marehemu siku hizi wanauwa wengine kisomi.Wanaweza kuuchunguza mwili pia wanaweza wasitambue ukweli ni upi. 

 

Maisha yetu tunayoishi kila siku

Na ni kawaida kwa maisha tunayoishi hapa duniani kuona, kusikia changamoto mbali mbali wanazopitia watu mbali mbali nani ukweli usiopingika kuwa ukiona wewe unachangamoto furani basi ujue kuna mwenzako anapitia changamoto, shida kama yako au zaidi ya hiyo kwa unayopitia. Tena ukitaka kujua, kuona tembelea mahospitalini uone watu wanavyopitia shida, magonjwa, changamoto mbali mbali.Na changamoto hizo hazichagui mtoto, kijana, mzee.

 Baadhi ya changamoto zinazopelekea watu kujiua, kujinyonga,  kwa nchi mbali mbali

  • Mambo ya mapenzi. (Fumanizi, ujauzito kukataliwa, kukataliwa na mpenzi wa kike au kiume, kubakwa, lawitiwa,kiungo fulani cha    mwili kutofanya kazi ipasayo, kutalikiana, kusalitiwa )
  • Maradhi sugu (Pumu, kisukari, Ukimwi, ugonjwa wa akili, kansa, kifafa).        
  • Wenza kufumaniana na kugundua kuwa mwezi mmoja  kiume ana tabia za ushoga au kufumwa kwa mwenza wa kike kuwa na tabia ya usagaji ambayo haikujulikana hapo kabla.
  • Ulevi kupindukia na matumizi ya madawa haramu ya kulevya
  • Maisha (Kufukuzwa kazi, msongo wa mawazo, kufeli mtihani, madeni sugu na kuyumba          kiuchumi, kukata tamaa,kusemwa na kusimangwa)
  • Kusikia sauti za watu wasionekana kwa macho ya nyama wakimshawishi muhusika     ajiue, kuumbuliwa kwa jamaa wa karibu katika uchawi.
  • Kurithi, historia ya mambo kama hayo kwa baadhi ya familia.
  • Kifungo cha miaka mingi kwa mwenzi mmoja wa kike au kiume.
  • Kuna watu wanaua watu wengine afu wanawaninginiza ili watu wakija kuangalia waseme wamejinyonga, hao waliofanya jambo hilo la kinyama hawajaonwa na mtu lakini wameonwa na mmoja aonaye kila mahali ni Mungu na hawezi kuwaacha hivi hivi watapata mshahara wake ambao ni mauti ya milele.
  • Wengine wanapiga risasi wengine na wao kujiua, jambo ambalo hata shetani mwenyewe hawezi kulifanya, kama shetani angeweza kufanya basi leo hii tusingekuwa na shetani na malaika na mapepo wake, vibwengo na majini na vinyamkera.
  • Je huna dini wewe? kwa nini usiwaone viongozi wako wa dini ili wakuombee, au nenda kwa wazazi au walezi , marafiki wa karibu unaowaamini? Watakutunzia siri? Marafiki ni watu tulionao karibu tunaoshirikiana nao katika shida na raha, pia ni muhimu katika maisha kuwa na rafiki unayemuamini, kushare changamoto na mwenzako ni njia moja wapo ya kuutua mzigo lakini pia maandiko yanasema tumtwishe Yesu Fadhaa zetu, je umemshirikisha amekujibuje? (1Petro 5:7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.)
  • Ukijiua ni sawa sawa kabisa na kuua umemtenda Mungu dhambi na unastahili adhabu, kiboko cha Mungu. Maandiko yanasema mshahara wa dhambi ni mauti, tena mauti ya milele. (Warumi 6: 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.)
  • Kila shida iliyopo duniani wewe sio wa kwanza kuna wengine wanashida zaidi ya yako mara tatu mpaka  nne zaidi, hawajakata tamaa na wanaishi duniani, lakini pia mafanikio mengine hayaji kirahisi rahisi mpaka upitie changamoto fulani.
  • Kila mtu yupo duniani yupo kwa kusudi fulani la kiMungu, yeye ndio ameruhusu uje duniani na yeye ndiye atakaye ridhia wewe uondoke katika dunia hii baada ya kuona kusudi lake alilolipanga limekamilika. (Yohana mt 15:1-2 1mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.2Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.)

  • Kuna baadhi ya watu wapo duniani tena wengine ni ndugu wa karibu au mzazi au mtoto wana wachawia wenzao wanawatesa wenzao kwa kuwapatia ugonjwa wa akiri, magonjwa yasiyo tibika, au mlogwaji kujichukulia uamuzi wa kujiua ili mlogaji apate utajiri wa chap chap ila Mungu anajua kila kitu utakuja toa hesabu. Kuna nyumba kijana wao wa kwanza ni wa kitandani muda wote, siku moja mama mzazi wa huyu kijana mgonjwa aliniita nikamwone, baada ya kwenda kumuona da ni huruma kwa kweli huwezi amini , Nilitaka kufanya huduma nikasikia sauti inaniambia "baba mtu anahusika na mchezo mchafu huu" hapo hapo nikaanza kuona vikwazo toka kwa mzazi wa kiume, sikuendelea na maombi nikajiondokea kimya kimnya sikurudi. Sijaonana na mama mtu siku nikimwona nitamwambia aende kanisa la jirani.
  • Nyumba za ibada zikiwa chache kuliko nyumba za starehe bar, Casino, Vijumba vya waganga wa kienyeji ni rahisi matukio ya kujiua kuongezeka katika jamii husika. 
  • Utandawazi wa siku hizi wa kuwapa uhuru uliopitiliza watoto wetu tuliowazaa wa kuangalia internet au chochote kinacho oneshwa katika internet na Tv, sio kitu kizuri kwa watoto, sio hivyo tu bali siku hizi kuna moves nyingi nyingi baadhi sio nzuri kwa watoto unaweza kukuta kuna moves watu wanapigana bastola, visu, mishale baadhi ya vitu watoto wakitazama kwa muda mrefu inaweza kuwaathiri na kujikuta wakitaka kufanyia zoezi kile kitu walichokiona luningani au kwenye internet. Kuna moves fulani fulani origin yake ni kwa mawakala wa shetani wamepanga kupenyeza vitu fulani fulani kwenye jamii yetu kwa siri.
  • Binadamu wote siku moja tutakufa, na kila mtu akifa ana takiwa kutoa ripoti yake mbele za Mungu, wewe uliyejinyonga utatoa taarifa gani? (Warumi 14: 12 Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.)

 

Katika utafiti uliofanywa na shirika la afya ulimwenguni (WHO) na matokeo yake kutangazwa kuwa taarifa rasmi ya umoja wa mataifa (UN) Mwaka 2014 inaeleza kuwa katika kila sekunde 40 mtu mmoja duniani hujiua. Pia kila Septemba 10, ni siku ya kimataifa ya kuzuia kujiua ambapo amasisho za kuzuia kujiua zinatolewa kote duniani.

 

Kabla ya kujiua tafakari yafuatayo kwa umakini

 

Hata watu unaowaona wanaishi kwa raha leo ujue ya kuwa kuna kipindi katika maisha yao walipitia mateso furani, kwa hiyo taabu au mapito ni ya muda na Mungu yupo pamoja na wewe sio kwa sababu hakupendi. lakini ujue ya kuwa wakati mwingine Mungu huruhusu taabu. mateso na changamoto upitie ili baadaye aje kuwaaibisha waliokucheka na kukudharau kwa hiyo ndugu usife moyo.

Kwa nini ifike mahali Mungu ajute kwa kutuumba, akasirike kwa ajili yetu sisi binadamu na kughairi kuwa alituumba, kwa nini tumsumbue Mungu muumbaji? Mungu ambaye ambaye hapendi kelele.

Mtu aliye kwenye mateso makali  kuliko wote

Kwenye biblia kuna mtu ametajwa aliye kwenye mateso makali yasiyo elezeka ni kulia tu muda wote, huyu ndio angetakiwa atamani kujiua ingeeleweka, lakini hatamki swala la kujiua iweje wewe duniani utamani kujiua? Embu msome afu mlinganishe mateso yake na yako unayopitia

(Luk 16: 19 – 31 19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya Yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa Yule masikini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa akazikwa.23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sis na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. 31 Akamwambia, wasipowasikia Musa na Manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.)

Mtu huyo yupo kwenye mateso ya moto usiozimika na kiu ya ajabu ya kutamani kuburudishwa   japo na tone la maji bila kulipata. Iweje leo wewe mtu unaye ishi duniani na kufurahi katika dunia yenye uwepo wa Mungu, ulinzi wake, wema wake, upendo wake wa kutufia msarabani, neema yake, furaha yake, roho wake na mema yake mengi mengi kila iitwapo leo. Mungu anatutendea  mema mengi kila siku, iweje leo Mungu kuruhusu baya moja tu kwako likupitie ulalamike sana hata upelekee kukufuru? Ya kutaka kujiiua au kujizuru?

 (Ayubu 2:10 10 Lakini yeye akamwambia, wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya ? katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.)

 

Sisi kama binadamu sio sawa kumlalamikia Mungu na Badala yake ni kushukuru kwa kila jambo linalotendeka, kwa sababu katika kila jambo Mungu ana makusudi yake ambayo ni yeye Mungu anayejua peke yake.Pia katika kila pito au changamoto mtu anayopitia ujue kuna mtu anapitia changamoto nzito zaidi duniani hapa, Yeye kama mfanyanzi na sisi ni udongo tumwache Mungu afanye mapenzi yake.

Tamati namalizia kwa kusema ili kuondokana na nia ovu ya kujiua/ Kujinyonga Omba Toba mbele za Mungu akusamehe nia yako ovu hiyo, Mungu ni mwaminifu yupo kila pahali atakusaidia, lakini pia ukishindwa mwite mtu unayemuamini akusaidie katika tatizo, shida hiyo, Bila shaka Mungu atafanya njia au mlango wa kutokea na kushinda hilo jaribu,(1 Kor 10:13 Jaribu halikuwapata ninyi,isipokuwa lililo  kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kushahimili).  nawe utaishi kwa furaha na amani kama wengine, Ubarikiwe na Bwana Yesu.


Kama utakuwa tayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.


“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”


Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.

1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku. (Warumi 10:17), (Wakolosai 3:16)

2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike   5:17)

3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri  wokovu na      kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25)

4.  Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione aibu, acha uvivu, tafuta pesa, Mungu katoa                         agizo tangu kale, Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo hivyo,   (2Thesalonike                       3:10)

5. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani. (Ufunuo 3:11), ( Mwanzo 3:1-19) (1Petro 5:8)

6. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) ,( Kolosai 4:16)

                                                                           Ni mimi

Mtumishi Emmanuel T.M.Omari
injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com




 

 

 

 

 



Monday, August 29, 2022

KUOMBEA WENGINE NA UFAHAMU WA ROHONI

 


(Matendo ya mitume 12:1- 19 Soma) Petro amefungwa minyororo chini ya ulinzi mkali

Katika Jumuiya, ushirika aliokuwa akisali Petro, Yakobo na Roda (dada wa kazi) Kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili ya Petro.

Kwa maombi ya Wanajumuiya, Wanaushirika Petro anatolewa gerezani kiajabu na malaika wa Mungu.

Anafika jumuiya, ushirika aliokuwa akisali Petro akawakuta wenzake wanasali kwa bidii ili Petro aachiwe.

Yakobo alichinjwa kwa sababu kanisa wanajumuiya, washirika walikuwa hawaombi, hata kama walikuwa wanaomba sio kwa mzigo.

Wakati mwingine tukipata changamoto ndo sisi binadamu tunaamka, wakati mwingine changamoto zinatuamsha.Pia Mungu anaweza ruhusu changamoto fulani au taabu ikupate ili usibweteke, (2Wakoritho 12: 7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.)embu waza u serious wa maombi kwa mtu anayeishi katika nchi yenye vita kila wakati kama Sudan na userious wa maombi kwa mtu anayeishi katika nchi yenye amani kama Tanzania.

Ulimwengu wa roho upo na unafanya kazi na ndo una nguvu kuliko huu ulimwengu huu wa mwili.

Ulimwengu wa roho upo na una sehemu mbili kuna upande wa Mungu na upande wa shetani

Karibu matukio yote yanayotupata au tunayopitia kawaida yanaanziaga rohoni kwanza kabla ya kuonekana mwilini. Au kwa lugha nyingine kila tukio baya lililotokea katika ulimwengu wa mwili lilianzia ulimwengu wa roho wa Shetani na kila tukio zuri unaloliona limetokea katika ulimwengu wa mwili lilianzia ulimwengu wa roho upande wa Mungu.

Matukio mengi liwe jema au baya  kabla ya kutokea mwilini Mungu anakuwa ameshayaona katika ulimwengu wa roho kwa neema yake ana uwezo wa kumfunulia mtu wake ili kuzuia madhara au kuruhusu jema  kwa jamii husika Mungu anatizamaga mtu wake ili amshirikishe. Siri ya Bwana ipo kwao wamchao.

Katika kitabu cha Esta tunaona Esta akimwambia mjomba wake Mordekai kuwa wamuombee kwani anategemea kuenda kwa mfalme kinyume na taratibu ili kuokoa Wayahudi wasiuawe.( Est 4: 15-16 Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai, Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa kwa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa Mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.)

Katika Jumuiya, Ushirika  alikokuwa  akisali Petro, Yakobo na Roda Kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili ya Petro.

Pia Yesu mwenyewe akiwa bustanini Gethemane alikuwa akiwaombea wanafunzi wake,ingawa wanafunzi wake walikuwa wakikoroma hawamuombei, (Marko 14:41 Akaja mara ya tatu, akawaambia, Laleni sasa mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama,Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi. lakini pia Yesu ameenda mbinguni kwa Baba huko pamoja na kutuandalia mahali, anatuombea pia.)

Musa baada ya Wana wa Israeli kukosa, Mungu alikusudia kuwafutilia mbali Musa akaomba kwa bidii kwa ajili ya wa wa Israeli Ili Mungu awasamehe uovu huu, Mungu akasikia akasamehe uovu wao.

 (Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.)

Kwa kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi basi mwana wa Mungu embu changamka omba kwa ajili ya wengine, pia kuna thawabu ukimuombea nabii kwa kuwa ni Nabii utapata sehemu ya thawabu ya Nabii, kwa kuwa kila mtu duniani ana sehemu ya thawabu katika uzima ujao ukifanya jambo jema kwa ajili yake haitakupotea thawabu yako Mungu ni mwenye haki.

Mungu anaongea na kila mtu kumjuza mambo ya mbele haijalishi ni mcha Mungu au la tatizo inaweza kuwa tafsili, mfano wa mtu ambaye Mungu aliongea naye shida ikawa tafsili ni pale Yusufu alipotiwa gerezani mnyweshaji wa mfalme an muokaji walivyoota ndoto wakiwa gerezani, wakashindwa kuifasili ila Yusufu aliweza kuifasili (Mwanzo 40:1 – 13 Soma)  pia kwa tukio hilo la Yusufu linatufundisha kuwa wakati mwingine Mungu huongea na wengine kuhusu wewe kwa kujua au bila kujua ili kupita katika changamoto fulani, ndo Mungu alivyo huwezi kuhoji sana ndo Mungu utaratibu wake huo.

Wakati Yesu amezaliwa kulikuwa na mtumishi wa Mungu ambaye Mungu alikuwa anamtumia kuandaa mazingira mazuri ya Yesu kuzaliwa, huyu mtumishi alikuwa akiomba kwa bidii kwa ajili ya Yesu, na Mungu alimtunza hakumuondoa duniani mpaka aje kushuhudia live huyo mwokozi wa ulimwengu, na siku alivyozaliwa mtoto Yesu, Roho Mtakatifu alimuongoza huyu mtumishi mpaka hekaruni akamuona Yesu, akashukuru na kusema  sasa Bwana wamruhusu mtumishi wako aende kwa amani kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu ... (Luka mt 2:29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, kwa amani kama ulivyosema.)

Wakati Yesu anawaaga wanafunzi wake anaenda mbinguni aliwaambia kuwa anaenda kuwaandalia mahali, jambo jingine ni kuwaombea akiwa kule mbinguni, kwa hiyo kuombea wengine ni jukumu la kila mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo, na kuombea mtu mwingine ni bure, sio mpaka posho. Kama wanavyofanya manabii wa uongo wa siku hizi za mwisho, hata maandiko yana tushuhudia yakisema tumepewa bure, tutoe bure. Mungu ni wa wote wenye mwili matajiri kwa masikini.

Ushindi wa Joshua Vitani ulitokana na maombi ya Musa pale mlimani  (Kutoka 17:8 – 15 Soma)

Pia sehemu nyingi katika  maandiko zaidi ya moja imeandika mpende jirani yako kama nafsi yako (Mathayo 19:19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, mpende jirani yako kama nafsi yako.)

Kabla ya Sodoma na Gomora kuchomwa moto Mungu alikuwa akihojiana na Abrahamu, Abrahamu alikuwa akiwakumbuka watu wa miji hiyo miwili mikubwa kwa kutaja idadi ya watu wenye haki 50, 45,40,30,20 mpaka 10 kama idadi hiyo itakuwepo katika nchi bado Mungu utahukumu? (Mwanzo 18:23 – 33 Soma)

Kwa kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi basi mwana wa Mungu embu changamka omba kwa ajili ya wengine, pia kuna thawabu ukimuombea nabii kwakuwa ni Nabii utapata sehemu ya thawabu ya Nabii, kwa kuwa kila mtu duniani ana sehemu ya thawabu katika uzima ujao ukifanya jambo jema kwa ajili yake haitakupotea thawabu yako Mungu ni mwenye haki.

Kuwakumbuka wengine kuna Baraka zake sisi kama binadamu tuna tofautiana nguvu za mwili hata za rohoni, tuwabebe wengine unaowajua na usiowajua Mungu mwenye haki hatakuacha hivi hivi tu (Zaburi 40:1 Heri amkumbukaye mnyonge; BWANA atamwokoa siku ya taabu.)

(Warumi 15:1 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.)

Sio hivyo tu hata Mfalme suleimani baada ya kuchaguliwa awe Mfalme wa Israeli alitokewa na Mungu katika ndoto, alivyoambiwa aombe chochote, alimwomba Mungu ' Kwa hio nipe mimi moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?" akapewa hekima Mungu akambariki double double kwa kuwatanguliza wenzake kwa Mungu wake. (1 Wafalme 3:5 -14 Soma)

Paulo mtume katika makala zake karibu zote amekuwa akimaliza kwa kusema upendo wa Mungu Baba na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote, ni namna moja wapo ya kuombea kuwatakia mema wengine kama watu wa Mungu.

Kwa hiyo kama mkristo  jifunze kuombea wengine mf.Yatima, wajane, wafungwa, wagonjwa sehemu mbali mbali hata kama huwajui au huna undugu nao huo nao ni utumishi wa Mungu unaonekana ni kitu kidogo machoni pa wanadamu ila kwa Mungu ni mkubwa sana, utumishi sio mpaka madhabahuni tu, pia tupo hapa duniani ili kumzalia Mungu matunda pamoja na kufanya kazi naye ukijizoeza kuombea wengine utajikuta Roho Mtakatifu akikuongoza kuombea mambo mbali mbali specific,na utabarikiwa na kuongezewa katika akiba yako ile iliyowekwa katika uzima wa milele.

Tusichoke kutenda mema, tusichoke kuombeana, sehemu nyingine maandiko yanatutia moyo kwa kusema tuombe bila kukoma. Ombea viongozi wa kiroho (Wachungaji, wainjilisti, mashemasi n.k) Ombea viongozi wa kimwili (Rais wa nchi, Mawaziri, wabunge, wajumbe, madiwani n.k) Kawaida Shetani akitaka kupiga kundi ana lenga hasa ampige kiongozi, sababu anajua nyuma ya watu hao kuna wengi, Imeandikwa (Mathayo 26:31 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga Mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.)

(I Wafalme 22: 31 – 33.

31 Basi mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru wakuu wa magari yake thelathini na wawili, akisema, Msipigane na mdogo wala mkuu, ila na mfalme wa Israeli peke yake. 32 Ikawa wakuu wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Huyo ndiye mfalme wa Israeli Wakageuka juu yake ili wapigane naye; naye Yehoshafati akapiga ukelele. 33 Ikawa, wakuu wa magari walipoona ya kuwa siye mfalme wa Israeli, wakageuka nyuma wasimfuate.)

Kwa hiyo tujenge mazoea ya kuombea Nchi yetu, tutubu dhambi za watu wake na machafu nyote yanayotendeka kwa siri, sababu tusipoombea kiboko chake na sisi pia tunaweza kupata upepo upepo wake, mfano katika nchi kama hakuna mvua sababu ya kumwaga damu za watu wasio na hatia, wote tunaathirika. Mtumishi wa Mungu Danieli aliombea wengine na kupata majibu yake haraka sana, ingawa kikwazo kilikuwa ni mkuu wa uajemi, Mungu alituma malaika wakaenda kumpambania. (Danieli 9:5-23 Tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu na watu wote wa nchi ...)

Mimi nakushauri nikiwa kama mtumishi wa Mungu wa kawaida tu ukipata wasaa wa kuombea mfano watoto wako, mume wako, mke wako, babu au bibi yako usirundikie maombi watu walio wa damu yako zaidi kuliko walio damu mbali na wewe, ujue kuwa kuna watoto wengi, wake za watu na waume za watu wako magerezani wanahitaji maombi yako, ukiomba kwa kuegemea upande mmoja inawezekana kabisa ukakosa baadhi ya mambo hiyo ni kanuni za kiroho. Pia kumbuka kuwa maandiko yanatushauri, tuwapende jirani zetu kama nafsi zetu.

Mimi binafsi mara kadhaa Roho Mtakatifu amekuwa akinishuhudia niombee mambo mbali mbali ya watu wengine, wengine nawajua wengine siwajui unaweza kukuta Roho Mtakatifu anakuongoza kuombea mtu mwingine  au tukio fulani la mbele tena kwa machozi, yaani picha inakujia unaona dhahiri bila chenga au unasikia kabisa unaambiwa ombea hiki, nami kama askari wa Bwana wajibu wangu ni kutii, jinsi Mungu alivyo wa ajabu.anawaambia watu wake kabla ya tukio husika kutokea, mambo kama haya sio rahisi kuelewa kwa mtu aliye nje ya Kristo hata humweleze vipi hataelewa ng'o. (Amos 3:7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya  neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.)

Ila pia katika maisha yangu binafsi mara nyingi najikuta huwa naombea zaidi watu wengine ndoa zao, kazi zao, watoto wao, uchumi wao, biashara zao kuliko hata kujiombea mwenyewe sijajua kwa nini ila nafanya kile ambacho nasikia kusukumwa kukifanya ndani yangu. 

Sio hivyo tu bali kwa waumini walioamini na kupokea kipawa cha kunena kwa lugha, sababu ahadi hii ni kwa wote waaminio, unaweza kuomba kwa lugha mpya, Roho akikusukuma kutoa machozi, bubujika mwana wa Mungu, hapa hakika hujui unayoyasema ila ni lugha ambayo Shetani huwa anang'ang'aa macho hajui kinachozungumzwa, ni lugha ambayo unaongea na Mungu mwenyewe direct, ni neema iliyoje? Mungu atupe nini tena? Nikuulize swali hivi kama una uhitaji, shida fulani ya kumwambia Rais au Waziri ni kitu chepesi au utapata mlolongo wa taratibu ndeefu na vikwazo kibao ili kuongea naye, unaweza ambiwa tatizo lako nenda ofisi fulani watashughulikia, ila Mungu yeye anatualika sote twende kwake na habagui cha ajabu huyu Mungu tunaenda kwake moja kwa moja tunaomba kupitia jina la mwanwe mpendwa Yesu Kristo, tena maombi yenu yanakuwa ni siri baina yenu nyie wawili hasa pale unaponena kwa lugha, lugha hii hata malaika wanaambulia patupu ni wewe na Mungu tu, (1Wakorintho 14:2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake). fursa ipo kwetu sote. Tuchangamkie fursa.

Kama utakuwa tayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.


“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”


Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.

1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku. (Warumi 10:17), (Wakolosai 3:16)

2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike   5:17)

3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri  wokovu na      kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25)

4.  Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione aibu, acha uvivu, tafuta pesa, Mungu katoa                         agizo tangu kale, Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo hivyo,   (2Thesalonike                       3:10)

5. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani. (Ufunuo 3:11), ( Mwanzo 3:1-19) (1Petro 5:8)

6. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) ,( Kolosai 4:16)



Barikiwa na Bwana

Ni mimi 


Mtumishi Emmanuel T.M.Omari

injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com