(Luk 17:3-4 Jilindeni;
kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara
saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.)
Kama utakuwa
umekumbuka kuwa ulikosana na ndugu, jirani yako wakati mwingine kukumbuka huku
ni Mungu anaongea nasi maana yeye njia zake hazichunguziki chukua hatua ya
kutengeneza haraka. (Mathayo mt 5:23 -24 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni,
na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako
mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kasha urudi uitoe
sadaka yako). Mungu wetu si wa machafuko anapenda amani, pia kuna sehemu amesema
tujitahidi kuitafuta amani tena kwa bidii na huo utakatifu ambao hapana mtu
atakaye mwona Bwana asipokuwa nao.
Mbele za Mungu dhambi
zote zina msamaha lakini sio dhambi ya kumkufuru (Roho Mtakatifu Marko 3:28 - 29 Amini, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa
wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho
Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa na dhambi ya milele). Usiwe
na hasira iliyopitiliza utampa Shetani mlango wa kukuingia na kukufanyia
atakacho, haijalishi kabila lenu mna asili hiyo embu ishinde hiyo asili maana
hakuna kisichowezekana. Kabila lako lisikufanye ukaikosa mbingu na nchi mpya, roho hii ya hasira haiwaachagi watu salama na shetani hakatagi tamaa upesi mpaka afanye
alichokusudia. Kuwa na hasira si dhambi, dhambi ni pale utakapoikumbatia mpaka
ikapelekea kuzaa matunda. Kaini aliambiwa na Mungu dhambi inakutamani lakini
yakupasa uishinde.(Mwanzo 4: 7 Kama
ukitenda vyema, hutapata kibari? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea
mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.)
Ukiwa hujasamehe unatembea, hujatengeneza na Mungu wako unaweza sababishia wengine madhara, kama ilivyotokea kwa Nabii Yona kusababishia wenzake kupoteza mali na usumbufu katika Safari yao toka Ninawi mpaka Tarshishi (Yona 1:5 Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi) Nabii Yona kesi/hasira yake na Mungu ilipelekea abiria wenzake na pia kwa kuwa roho ya hasira haikufanyiwa kazi kikamilifu ilipelekea umauti kutokea mapema. (Yona 4:4-8 Naye BWANA akasema, Je! Unatenda vema kukasirika…) shetani hamwogopi mtu yeyote hakumwogopa Yesu wewe ni nani? Musa mtumishi wa Mungu aliyefanya mambo makubwa katika historia ya wana wa Israeli. Alikuwa na roho ya hasira iliyojificha ambayo hakuifanyia kazi Kutoka 2:11-15 Musa alivyompiga Mmisri na kukimbia …hasira hiyo aliendelea nayo ikapelekea kumkosesha kuigia mji wa Kaanani pamoja na kuwa aliuona mji kwa mbali. (Hesabu 20:8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao) Kitendo cha Musa kufanya kinyume cha maelezo ya BWANA hasira zikamponza. Hesabu 20:9-12 Watu wenye hekima huwa wanashauri kama una hasira si vizuri kufanya jambo wala hata kuongea ni heli ukae kimnyaa kwa muda kabla ya maamuzi. Baada ya kifo cha Musa Mungu alindaa mtumishi mwingine ili kuwawezesha wana wa Israeli kumaliza safari.
Maandiko kuna sehemu
yanakiri kuwa unaweza kuishika torati yote vizuri lakini ukiikosea katika moja
ukawa ukekosa juu ya yote kwa hiyo tujitahidi iwe maombi yetu ya kila siku
kushinda huu udhaifu tuishitaki mbele za Mungu mtakatifu kwa kuwa yeye ana
nguvu kuliko shetani tutashinda sababu aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye
aliyeko katika dunia.
Kutosamehe kunachafua
roho yako, unaweza kuikosa Mbingu au Baraka mbali mbali toka Kwa Mungu.
Malaika ni wajumbe,
watumishi wa Mungu wanapotumwa kwako kukuletea baraka tofauti tofauti mbali
mbali sababu wenyewe wapo katika roho wanapo kuja wanaiona roho yako imechafuka
basi wanarudisha kile kitu walichokuletea wanaenda kukihifadhi kinakaa
kilipotolewa, kwa duniani hifadhi hizo tungeweza kuiita kabati, friji, store
mpaka utakapo kaa sawa sawa etc. ni kama vile wewe ni mzazi unakuja kwa mwanao
mdogo unatamani kumpa kitu kizuri, lakini ukute amejinyea, je utampa kile kitu
kizuri, si utaondoka na kumpa siku nyingine au atakapokuwa amejisafisha au
amesafishwa.
Mungu hawasikilizi
wenye dhambi maombi yao ni kelele
(Yoh mt 9:31 Twajua ya kuwa Mungu awasikii
wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kufanya mapenzi yake, humsikia
huyo) sifa zao kwa Mungu huonekana kama ni makelele.
Migogoro mingi katika
ndoa chanzo kikubwa ni kutosameana Mume na mke, mhhhhh.Kunyimana nyimana
vitu vilivyo haki katika ndoa, kukomoana. Mwanamke& Mwanaume kunyemelewa na
Shetani kuhusu kutafuta mbadala (Mpumbavu
huamua kwa haraka na, madhara yakamkuta) Shetani anazunguka zunguka akitafuta
mtu awe mwanachama mapepo nayo yanazunguka zunguka hayalali. (1Pet
5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba
angurumaye, huzunguka zunguka akitafuta mtu ammeze).
WATUMISHI WACHACHE
WALIOKIMBILIA TOBA BAADA YA KUGUNDUA KUWA WAMEKOSEA
i.
Daudi kwenye kesi ya Mkewe na Uria 2Samweli 12:13
ii.
Petro alivyomkana Yesu mara tatu kuwa hamjui Yohana mt 18:25-27 Baada ya
hili tukio hatumuoni Ptro akiomba msamaha kwa ajili ya tukio hili alilolifanya
la kumkana Yesu mara tatu (Yohana mt 21:15 Basi walivyokwisha kula, Yesu
akamwambia Simoni wa Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko
hawa?Akamwambia, Naam, Bwana , wewe wajua kuwa nakupenda.Akamwambia lisha wana
kondoo wangu. Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda?
Akamwambia Ndiyo Bwana wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia chunga kondoo
zangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda, wanipenda? Petro
alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu wanipenda? Akamwambia, Bwana,
wewe wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha
kondoo zangu.) Pamoja na kuwa Petro alikasirika bila kujua Yesu alikua
anamfungulia kifungo chake kutokana na kumkana Yesu mara tatu kwake baada ya
kukiri kwa kinywa chake akawa amepona.
BAADHI YA MATATIZO/
ATHARI ANAZOWEZA KUPATA ALIYE NA ROHO YA KUTOSAMEHE/KUWEKEZA
Mioyo yetu haikuumbwa ikae na uchungu, hasira, chuki. Ukikaribisha vitu hivyo unakaribisha Magonjwa, k.v. Presha, Msongo wa mawazo, Kichwa Kuuma, Vidonda vya Tumbo, Kuchanganyikiwa (Kuongea Peke yako), Ajari, Asilimia kubwa ya watu wanaojinyonga, kunywa sumu ni watu walioumizwa na uchungu uliopitiliza Yusufu baada ya kuonana na ndugu zake walio muuza alikumbuka mabaya aliyo tendewa, uchungu ukamjia akaomba aondolewe kila mtu ili aweze pata faragha ya kulia, kulia nako ni dawa kunasaidia kutoa uchungu wa moyoni, baadhi ya watu wanasema kama mtu hatalia katika matukio mbali mbali yanayotukuta wanadamu anaweza kupata matatizo fulani ya kiafya, kwa hiyo kulia kunasaidia kutoa sumu na kupunguza baadhi ya magonjwa.
(Yuda Iskariote Mt
27:5), Watu wengine wamekasirika wakajikuta wapo Kifungoni wanajuta.Petro hakuwekeza
kosa alilotenda la kumkana Yesu tena mara 3 alitubu na kuomba msamaha,
Akasamehewa. Naamini hata Yuda pamoja na kumsaliti Yesu kama angekuwa na roho
ya toba angeweza kusamehewa. Ila binadamu tuna tofautiana tabia tunaweza kuwa
hata mapacha lakini tusifanane kila kitu. Ila tuwe na moyo wa toba, toba na kunyenyekea na kurudi kwa mwenyezi Mungu na kutotubu ni roho ya kiburi. Na
Mungu huwapinga wenye kiburi (1Petro 5:5
Vivyo
hivyo ninyi vijana, watiini wazee.Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu,
mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi,lakini huwapa
wanyenyekevu neema.)
Kwa kawaida kati ya
watu wawili waliokoseana anayesamehe na anayesamehewa anayeumia zaidi ni
yule asiye samehe, sababu kila ukimwona mgomvi wako unakumbuka wakati labda
mwenzako alisha samehe, na kusahau siku nyingi, kwa hiyo usiposamehe ndio
unaumia zaidi.
Sala Ya Bwana Tunakiri
kuwa “Baba yetu uliye Mbinguni, utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe
Waliotukosea” Tunajifunga kwa maneno ya kinywa chetu wenyewe. Kama hutaki
kusamehe na kuachilia na Mungu naye hakusamehi ng’o nani anayeweza kuishi bila
msaada wa Mungu, bila ulinzi wake, upendo wake, neema yake? Ukihukumiwa kwa
kosa hilo siku ya siku ni haki yako sababu umekiri kwa kinywa chako mwenyewe.
Tuwe wepesi wa kuomba
msamaha kwa Mungu wetu, wenzi wetu hata watoto wetu, majirani, wafanyakazi
wenzetu n.k
Katika wanafunzi
aliokuwa nao Yesu, Yuda alimsaliti Yesu akakaa na uchungu hakuutoa ukamdhuru ,
Petro naye alimsaliti Yesu tena mara tatu. Yuda mara moja, Petro alimkana Yesu
mara tatu akatubu fasta. Akapata msamaha, sio suala la dhambi kubwa au ndogo
Mungu kwake hata dhambi iwe nyekundu husamehe kabisa. Mungu wetu aliyeumba
mbingu na nchi yupo mbali sana, lakini kwa uwezo wake yupo pia karibu sana
mwombe yeye akuwezeshe kusamehe, kwa nguvu zako peke yako huwezi. Yeye ni wa
huruma,na rehema na anatuvumilia kwa mengi atakuwezesha, maana hakuna jambo
lililo gumu la kumshinda yeye Mungu.
Tena pia tunaaswa
tukiwa na hasira sana au furaha sana tusiamue jambo, maana ni rahisi sana
kuamua kinyume na mapenzi ya Mungu (Mat 14:6-7 Hata ilipofika sikukuu ya
kuzaliwa kwake Herode,binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza
Herode.Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lolote, atakaloliomba.)
Wakati Bwana Yesu alipokuwa anaelekea Kalvali kuna kipindi alikuwa
anadhalilishwa, Yeye akiwa mwana wa Mungu ambaye Mungu amependezwa naye
aliulizwa swali akiwa na maumivu, alinyamaza kimnya, tujifunze kuwa wakati
mwingine kuna uponyaji katika kutojibu jibu au kukaa kimnya. (Mark 15: 4
-5 Pilato akamwuliza tena akisema,Hujibu neno? Tazama ni mambo mangapi
wanayokushitaki! Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu.)
Stephano Alipigwa na vijana waliofundishwa na Sauli Stephano” Alikufa huku akimwomba Bwana Usiwahesabie Dhambi hii, wasamehe Bwana. (Mdo 7:60 Alipiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii.Akiisha kusema haya akalala). Hapa kulala maana yake ni kufa.
Bwana Yesu pamoja na kudhalilishwa yeye akiwa kama
Mwana wa Mungu alikuwa na Jeshi kubwa la Malaika ambalo angeweza kuliamlisha
lifanye vyovyote, likafanya alidhalilishwa lakini akasema, "Bwana wasamehe
kwa kuwa hawajui watendalo".
Yusufu pamoja na kuwa ndugu zake walikuwa hawampendi na visa kede kede ikiwemo kumuuza ugenini lakini siku zikapita wakiwa na njaa walikimbilia kwa Yusufu wakihitaji msaada wa chakula wasife kwa njaa, Yusufu aliwajua ndugu zake lakini wao hawakumjua, aliwatendea mema nduguze.
Habari ya Yusufu pia
itufundishe jambo jingine hapa, kitendo cha Yusufu kutokasirika kutochukua
maamuzi magumu mf.kujiua kwa mabaya aliyotendewa na ndugu zake, kwake ilikuwa
ni mtihani ambao kushinda kwake imempelekea kuwa Waziri mkuu. Je wewe unajua
baada ya jaribu au mtihani huo Mungu ameandaa nini mbele yako? Kwa nini ukubari mwovu akuharibie na kuvuruga lile jema ambalo Mungu alikupangia
ulipate ukiwa hapa duniani, kabla ya yeye mwenyewe hajahitimisha uhai wako?
Hivi unajua kusudi la Mungu kukuleta, kukuweka hapa duniani? Kila Mtu aliyepo
hapa duniani yupo kwa kusudi fulani la ki Mungu, ndo maana utakuta wanaokufa
sio kwamba wana madhambi sana kuliko
sisi tunaoendelea kupumua.
Eliya alifanyaje ? Kama Eliya aliweza kuagiza moto kutoka Mbinguni uteketeze 50 Yesu si Zaidi! Eliya Mtu wa Mungu kama mimi, kama wewe tu wewe je? 2 Wafalme 1:10 Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka ukamteketeza, yeye na hamsini wake)
Kutoomba Toba ni
kiburi mbele za Mungu au wanadamu, maandiko yanasema Mungu huwapinga wenye
kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.sio hivyo tu lakini pia kusamehe ni kutii
agizo la Mungu, (Warumi 12:19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali
ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi
nitalipa, anena Bwana.)
Ukilipa kisasi unapingana na agizo la Mungu yaani huamini kuwa Mungu atafanya alichoahidi, yaani unamfanya kuwa Mungu ameahidi uongo hutaki Mungu akupiganie unajipambania mwenyewe.
(Mithali 17:13 Yeye arudishaye mabaya badala ya
mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake). Maandiko
yanaposema mabaya hayataondoka nyumbani mwake maana yake, nyumbani mwako
inaweza ikawa ni kwenye biashara yako, kazi zako, ndoa yako, watoto wako, yaani
kwa ufupi ni kwenye vitu vinavyokuhusu. Hilo ni neno la Mungu na neno la Mungu
ni kweli na amini.
Sio kwa sababu
maandiko yanasema Samehe saba mara sabini basi ndo iwe tiketi
ya wewe kukosea kwa makusudi , sababu utasamehewa kwa hiyo ukaamua
kuleta Makwazo ya makusudi. Maandiko yana onya juu ya mtu kama huyo aletaye
makwazo. Pia sio kwa sababu Mungu ni wa huruma au anasemehe si mwingi wa
hasira, tusijiachilie sana tuwe na tahadhari.
(Luka 17. 1 Akawaambia
wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja,
lakini ole wake mtu
yule ambaye yaja kwa sababu yake!)
Hata mtu akiamua kumpa Yesu maisha yake, sio kigezo cha
kutopata makwazo, makwazo yapo na hayataisha mpaka mwisho wa dunia, inapasa
tuyashinde, maana ndio njia ya msaraba hiyo, hakuna njia ya mkato, Yesu
alipitia wafuasi wake lazima nao wapitie.
Kama utakuwa
umetendewa neno ovu nawe ukaamua kulipa kisasi, hapo utakuwa ukifanya kitu
kinaitwa Kuhukumu, maandiko yanasema usihukumu, usije ukahukumiwa,
kisasi ni jukumu au kazi ya Mungu mwenyewe atalipa. (Mathayo 7:1 Msihukumu,
msije mkahukumiwa ninyi)
(Waefeso 4:26-27 '' Mwe na hasira, ila
msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka
; wala msimpe ibilisi nafasi.)
Shetani hawezi
kukushambulia mpaka umfungulie Mlango kupitia uovu hasira ni Mlango mmojawapo
anaotumia kushambulia, ili shetani apate nguvu na uhalali wa kukushambulia
wewe kama mwana wa Mungu lazima umvutie, utamvutia kwa kuwa na uwepo wa dhambi
moyoni mwako. Ndo Maana kama ni msomaji wa biblia utagundua pia wakati Yesu
alipokuwa akiwaombea, akiwafungua baadhi ya watu alikuwa akiwaambia umekuwa
mzima "Usitende dhambi tena" (Yoh 5:14
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya Hekalu, akamwambia,
Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo
baya zaidi) Na sababu nyingine
inayofanya watu wengi leo kushindwa kusamehe ni kwa sababu hawana Roho
Mtakatifu ndani yao pia hawataki kuomba msaada wa Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu akiwa ndani yako matunda yake
yataonekana tu hayajifichi. Na roho ya shetani ikitawala ndani yako matunda yake
yataonekana tu hata ujifiche vipi. Katika maandiko yanakiri kinywa cha mtu
hunena yale yaujazayo moyo wake (Luka Mtakatifu 6:45 Mtu mwema katika hazina
njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya mwili
wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo
wake).
Kisasi ni cha Mungu,
yeye atalipa, tena wakati mwingine Mungu hulipa tangia hapa duniani, Duniani
tunapita hatuishi milele sisi ni kama maua ya kondeni.
Abigaili, mwanamke mwenye hekima wa Israeli Agano la
kale, anatuwekea kielelezo kinachoonyesha matokeo ya kuomba msamaha, ingawa
aliomba msamaha kwa kosa la mumewe. Alipokuwa akiishi nyikani pamoja na
watumishi wake, Daudi, aliyekuja kuwa mfalme wa Israeli, alilinda kondoo za
Nabali, mume wa Abigaili. Hata hivyo, wakati vijana hao wa Daudi walipoomba
mkate na maji, Nabali aliwafukuza na kuwatusi vibaya sana. Daudi alikasirika na
kuongoza wanaume 400 hivi kwenda kumpiga Nabali na nyumba yake. Alipojua habari
hiyo, Abigaili alifunga safari kwenda kumlaki Daudi. Alipomwona, Abigaili
alimwangukia miguuni pake na kusema: “Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na
uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize
maneno ya mjakazi wako.” Kisha Abigaili akaeleza hali ilivyokuwa na kumpa Daudi
zawadi ya chakula na maji. Ndipo Daudi akamwambia: “Haya! Kwea kwa amani kwenda
nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako, nami nimeukubali uso wako.”—1Samweli
25:2-35. Baada ya siku 10
Nabali alifariki, alivyofariki Daudi alifanya mpango wa kumuoa Abigaili (Malipo
ni hapa hapa Duniani)
Solomoni Mukubwa (Ushuhuda)
Yeye ni Raia wa Kongo
anayeishi Kenya ni mtoto wa kwanza katika familia yao baba yao alipoongeza mke
mwingine Huyo mke Mwingine alimloga Solomoni Mukubwa alipokuwa na umli wa Miaka
12 akawa na uvimbe ambao ulipelekea kukatwa kwa mkono wake ili kunusuru uhai
wake, aliangaikiwa sehemu nyingi na wazazi wake bila mafanikio. Alijua kuwa
amelogwa na mama yake wa kambo baada ya yeye mwenyewe kukiri kuwa alifanya
hivyo. Huyu mama wa kambo naye aliokoka baada ya yeye naye kupata pigo ‘Mwanawe
alirukiwa na kijiti cha moto jichoni kilichopelekea jicho la mwanawe kuharibika
kabisa
(Malipo
ni hapa hapa Duniani) Solomoni Mukubwa katika kumbukizi ya tukio alilowahi kupitia ameimba wimbo unaitwa nimewasamehe
!!!
Usipende kuudhi watu ovyo ovyo watu wengine Wanampendeza Mungu kiasi ambacho ukikorofishana nao Malaika wananunua ugomvi unashangaa tu, unapata pigo hujui chanzo ni nini pigo inaweza kuwa gonjwa fulani, ajari au hata kifo kwa sababu zisizokuwa na majibu,sio watu tu kuna baadhi ya mataifa pia ukiyagusa umegusa mboni ya jicho la Mungu, unapigana nao bila kujua kuwa nyuma ya mtu au Taifa husika yupo Mungu. Hata katika ufalme wa giza nao kama kuna kufanana Fulani ukimfanyia kitu kibaya anayelindwa na majini unaweza kukuta majini wanakushambulia hata kukuua kabisa. Hata katika ulimwengu wa mwili wa wanasiasa sio vizuri kumsema kwa kumzalilisha mtu mwenye cheo mf.Rais wa nchi unaweza kushambuliwa na watu usio wajua, ukaingia matatizoni, kuwa makini chunga ulimi wako ndugu yangu kaka au dada. (1Petro 3:10 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya,)
Kaini na Habili
Kisa cha Kaini kumuua
Habiri ni hasira, uchungu ambao haukutubiwa (Mwanzo 4:3-15 Ikawa hatimaye Kaini aleta mazao ya ardhi,
sadaka kwa BWANA.Habiri naye akaleta mazao ya kwanza wa wanyama wake na sehemu
zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabari Habiri na sadaka yake ; …)Ukiwa
na hasira au uchungu moyoni mwako hata Sadaka yako
haitapokelewa mbele za Mungu ...(Mathayo 5:23 -24 Basi
ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno
juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na
ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako).
hata Maombi yako Mungu hayasikilizi sababu Mungu hawasikilizi
wenye dhambi.
Kuna watu tunaishi nao
hapa duniani ni wagumu mno kusamehe wenzao, hata umwombe msamaha yeye
atang'ang'ana na msimamo wa kutosamehe, watu wa jinsi hii unatakiwa ujiepushe
nao maana wanaishi chini ya laana hawatafanikiwa ng'o hata kama wanamafanikio
basi mafanikio yao yatakuja kupotea ghafla , Mungu si mwanadamu hata aseme
uongo, mshahara wa dhambi ni mauti.
uchungu
wote na ghadhabu
na hasira na kelele na matukano yaondoke
kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili
ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo
alivyowasamehe ninyi.(Waefeso 4:31,32)
Tuuangalie msaraba ili
tushinde, dunia yote imejaa makwazo, hata Yesu alisema " ulimwenguni mnayo
dhiki, lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu" (Yohana Mtakatifu
16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani
ndani yangu.Ulimwenguni mnayo dhiki ; lakini jipeni moyo ; mimi nimeushinda
ulimwengu.)
Sala:
" Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi. Sasa
nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha ... (zitaje mbele za
Mungu) niwezeshe kutozirudia kabisa nijaze na Roho Mtakatifu wako aliye mwalimu
na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu,
uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu Kristo kwa
kuniokoa" Amen.
Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha utakuwa umekwisha
okolewa, umeongoka, umezaliwa mara ya pili. Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu
Kristo,
Vifuatavyo ni msaada kwako ili upate kusonga
mbele na kuukulia wokovu.
1. Soma neno la Mungu Biblia Takatifu kila siku (Warumi 10:
17) na (Wakolosai 3: 16).
2. Sali asubuhi, mchana na
jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1 Wathesalonike 5:17)
3. Kama sehemu unayomwabudu
Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokili
wokovu na kutoa mafundisho ya kiroho ili
upate kuukulia wokovu (1Petro 2:1-2)
(Waebrania 10:25).
4. Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione
aibu, acha uvivu, tafuta pesa, Mungu katoa agizo tangu kale,Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo hivyo (
2Thesalonike 3:10)
5. Usikubali
kuusikiliza uongo wa Shetani (Ufunuo 3:11), (Mwanzo 3:1-19) na (1Petro 5:8).
6.
Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani
anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya
leo (Ufunuo 22: 18), (Kolosai 4:16).