Friday, January 10, 2014

MUNGU HAJAZAA WALA HAJAZALIWA !!!





 
Mungu wa Imani nyingine wasio  wakristo ni kweli hajazaa, hajazaliwa hana uwezo wowote yupo yupo tu.
Yehova Mungu wa wakristo yeye amezaa aliutuma ujumbe kwa kumtumia malaika ili aende kwa Bikira Maria kumtaarifu (Luka Mt.1:26-27) Mwezi wa sita, Maraika Gabriel alitumwa na Mungu aende mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali Bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbali ya Daudi; na jina lake Bikira huyo ni Maria,kuwa atachukua mimba kwa uwezo wa kiungu ambao haijawahi kutokea hapa duniani na kwa sababu yeye ni Mungu ana uwezo wa kufanya jambo lolote anaweza kuamuru hata mawe yawe watoto ikatokea hivyo. Anaweza kuamuru mtu aliye hai akawa mfu au mtu mfu akawa hai na ikatokea hivyo. ( 1Kor 9: 20-22) Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi,ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria ) ili niwapate walio chini ya sheria kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria ,(si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo) ili niwapate hao wasio na sheria kwa  wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge.Nimekuwa hali zote kwa watu wote ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.Ukitaka kuwapata watoto inakubidi nawe ujifanye mtoto ili kuwapata watoto japo kidogo bila hivyo hutawapata ng’o, Ukitaka kuwapata wenye pesa inabidi nawe ufanane fanane nao japo kidogo bila hivyo hutawapata hata kidogo.Kama hukutaka Mungu amtumie mwanadamu aliyemwumba tena mwanamke tu ambaye anaonekana kama kiumbe dhaifu kwa baadhi ya watu ulitaka Mungu atumie kuku au mbuzi ili kufikisha ujumbe kwa wanadamu aliowaumba kwa kuwagharamia sana, je kuku au mbuzi angekubarika miongoni mwa jamii ya wanadamu? Ni nani angekubali kusikia na kutilia maanani ujumbe ambao ungetolewa na kuku au mbuzi?  Tungeweza kukubari na kutii kile (ujumbe) ambao Mungu angeutoa kwa kutumia kuku au mbuzi? Na kutii, iwapo kama kwa kutumia binadamu tu mpaka leo watu wengi bado wanakejeli kwa namna mbali mbali ule ujumbe ambao Mungu aliutelemsha kwa kumtumia Yesu?
Hata hivyo Mungu hakulazimika kuangaika sana kumtafuta mtu arudi katika njia yake ila ni basi aliamua tu, Mungu kwetu sisi binadamu hufanya vile aonavyo kuwa sawa kwa mtazamo wake sisi ni binadamu tu hatupaswi kuhoji, kulalamika sana mambo atufanyiayo Mungu, vinginevyo huenda tukaonekana tuna pingana na mipango na maamuzi yake, sisi ni udongo tu mbele za Mungu, yeye ni mfinyanzi (Yer 18:5-6) Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,Ee nyumba ya Israeli, je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda?asema Bwana. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.
Historia ina kawaida ya kutufundisha wakati uliopo, uliopita  na wakati ujao.Vitu vingine Mungu anavyovifanya kwa wanadamu hupita fahamu zetu hata uambiwe akiri hufika ukomo wa kufikiri.


BAADHI YA MAAJABU AMBAYO MUNGU ALIYAFANYA KATIKA DUNIA HII TUNAYOISHI SASA

1. Aliigawa bahari ya Shamu watu wakapita kati kati yake (Zab 66:5-6)

2. Mungu aliwahi amuru mwanamke wa miaka 90 azae mtoto ikafanyika hivyo  (Mwanzo 21:2)

3. Mungu aliwahi ruhusu punda mnyama aongee sauti ya kibinadamu kitu ambacho hakitegemewi kabisa (Hesabu 22:28-30)

4. Mungu aliumba nyota ,mwezi, jua vingine vinavyo onekana ambavyo bado kugunduliwa na visivyo onekana.

5. Mungu aliwahi kuiangamiza dunia yote kwa maji na kubakisha watu nane tu walio mpendeza moyo wake.(1Petro 3:20)

6 Mungu aliwahi simamisha Jua kwa muda (Yoshua 10:13)

7. Mungu aliwahi kuingilia mawasiliano ya mtu na mtu wasielewane ili kusudi lake    litimie.(Mwa 11:1- 9)

8. Mungu anaweza fanya mvua inyeshe katika nchi na mafuriko yakatokea, pia anaweza ruhusu mvua  isinyeshe na kukatokea ukame katika nchi yoyote aitakayo yeye.(1Fal 18:1)

9 Mungu anaweza kufanya muujiza wa samaki wawili na mikate mitano wakala zaidi  ya watu 10,000 watu wakala wakashiba na kuisaza.(Yoh Mt 6:1-13)

10. Mungu anaweza amuru jabari/jiwe kubwa litoe maji ikafanyika hivyo (Hesabu 20:8 -11)

11 Mungu anaelewa lugha zote za hapa duniani, hata lugha za wanyama, ndege,miti, bahari ,wadudu  etc   (Zab 96::11-12), (Zab 98:7-8)

12 Kwa uweza na nguvu zake anatawala milele yote kwa haki tena ni mtakatifu mno mfano wake duniani, mbinguni hakuna. (Zab 66:7)

13. Mungu aliwahi kumfufua Yesu aliyekuwa amekufa, Lazaro naye alifufuliwa tena alikuwa ameshaanza kuoza na kunuka (Mark 8:31)

14  Alimgeuza jambazi sugu Paulo aliyekuwa akiitwa Saul kutoka katika ufalme wa giza na kumuingiza katika ufalme wa nuru yaani wa Yesu Kristo.(Mdo 9:1-22)

15. Mungu huyo huyo anaweza kumtumia mtu mwingine unayemdhania kuwa hafai, taka taka, kafiri kukuletea habari za ukombozi wa roho yako ukikubari ni kwa faida yako na ukikataa pia ni kwa hasara ya nafsi yako (1Kor 1:27)

16. Mungu aliwahi ruhusu ardhi ifunue kinywa na kufumba iwameze wale walio mkosea kitu ambacho ukifikiria kwa akiri ya kawaida akiingii akirini, unashindwa kuelewa kabisa.(Hes 26:10)

17 Mungu ana uwezo wa kukuona wewe usimuone, pia ana uwezo wa kurekodi matendo yako yote mabaya na mema na kuyaweka katika CD yake ya ki ungu na kuyatumia kama ushahidi wa siku ile  ya   hukumu itakapo fika.Hata jiwe linaweza kutoa ushahidi kwa Mungu (Yoshua 24:27)

18. Mungu ana uwezo wa kuruhusu ushirika wa mwanamke na mwanaume azaliwe mtoto, kwa nguvu  na uwezo wake, pia anaweza ruhusu mwanamke azae bila ushirika wa mwanaume kama ilivyo kwa bikira Mariamu (Mathayo 1:23/ Isaya 7:14) Ni kamuujiza cha mtoto mbele za Mungu.Mamaye Yesu     pia aliuliza litakuwaje jambo hili wakati sijui mume…? Malaika/Mungu baada ya kujieleza mwisho kasema hakuna jambo la kumshinda Mungu, pia maana yake ni Mungu anaweza kufanya lolote atakalo, hashindwi na lolote. Hapa inamaliza maswali yote ya inawezekanaje kuzaa bila mwanaume, kwa mwelewa.(Luka mt 1:34-38)

19. Aliokoa na anaendelea kuokoa kila siku watu wa Imani zote ambao walikuwa hawamjui Yesu baada      ya kuujua ukweli wa Wokovu (Waebrania 3:7-8)

20. Mungu pia haimtishi iwapo idadi kubwa ya binadamu/watu wataamua kwa hiyari yao ku tomfuata Yesu jina litupasalo kuokolewa kwalo wenyewe na kumfuata mfalme wa anga Shetani na mwisho  kuangamia katika moto wa jehanamu. (Mwa 9:3) Alishawahi kuiangamiza Dunia na kuua watu wote    kwa Gharika na kubakisha watu nane tu, pamoja na watu kulia na kusaga meno haikusaidia.

21. Mungu halali hasinzii akitulinda, pamoja na ukaidi wetu, wakati sisi binadamu hulala, husinzia, tunapolala adui ni rahisi kutuvamia ni ulinzi wa Mungu tu utupao uzima siku hadi siku (Zab 121:3-5) Ayu 1:7-10)

22 Katika ulimwengu tunaoishi kuna nyota nyingi mabilioni kwa mabilioni lakini Mungu zote azijua tena kwa majina na idadi ya nywele za vichwa vyetu vyote inajulikana, binadamu duniani tupo wangapi? (Luk 12:7) (Zaburi 147:4)

23 Mambo aliyofanya Mungu na anayotufanyia sisi binadamu ni mengi mno hayaandikiki katika karatasi yakatosha hayahesabiki (Yoh 21:25) ingawa Shetani kwa dharau zake kwa Mungu anashawishi binadamu wayaone yote aliyofanya Mungu ni maajabu saba ya dunia. Hakuna maajabu     saba ya dunia kuna maajabu zaidi ya maelfu ya Mungu sio ya dunia ni ya Mungu Mtakatifu, unapotaja Mungu unakuwa umemsifu Mungu, unapotaja dunia unakuwa umemsifu mungu wa dunia.

24 Mbingu ni kiti chake cha enzi, duniani ni mahali pa kuweka miguu, Ukuu wa Mungu umepita ufahamu wa binadamu (Isaya 66:1)

25 Mungu mbingu hazikutoshi wala mbingu za mbingu. Ewe mwanadamu kwa akiriyako utamlinganisha na kitu gani, kama si kumwacha tu Mungu aitwe Mungu.(2Nyakati 6:18)

Mungu akipa kila kiumbe chakula chake, ulimwenguni hapa kuna viumbe vingapi? (Zab 136:25) Unataka kumfananisha na nani hapa duniani? Na Rais yupi, tajiri yupi, mfalme yupi?


BAADHI YA SABABU KWA UCHACHE, KWA NINI YESU NI MWANA WA MUNGU KWA USHAHIDI WA  MAANDIKO

1.     Manabii

Walitabiri walitabiri kuzaliwa kwake kabla (Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atatokea mmoja...), (Mathayo Mt 2:6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israel) , (Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli) (Mathayo 1:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sharia, yaani, adili, na rehema,na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.) Mungu ana utaratibu wa kuwajulisha rafiki zake, baadhi ya mambo kabla ya kuyafanya (Mwanzo 18:17 Bwana akanena Je! Nimfishe Ibrahimu jambo nilifanyalo, ; (Amosi 3:7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake) (Yohana mt 15:15 siwaiti tena watumwa kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewataarifu. Hakuna msingi thabiti wa Imani kama wa Manabii na Mitume (2Nya 20: Wakaamka asubuhi na mapema …

(Waefeso 2:20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni)

2.      Mungu mwenyewe, Petro, Yohana na Yakobo

(Yohana mt 3:16 Kwa maana jisi hii ungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee.)

(Mathayo 17:15 Alipokuwa katika kusema, tazama wingu jeupe likawatia uvuli ; na tazama sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye).

3.     Yesu mwenyewe

(Yohana Mt 10:36 Je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru? ; kwa sababu nalisema , Mimi ni mwana wa Mungu? Naye akajibu ni nani? Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia, umemuona, naye anayesema nawe ndiye. Sio hivyo tu bali Yesu mwenyewe alikiri kuwepo kabla ya kuzaliwa duniani aliposhiriki utukufu wa Mungu (Yohana mt 17:5  tena alisema, kabla babu yake Ibrahimu kuweko alikuweko alikuweko kama niko ambaye niko (Yohana Mt 8:58, Kutoka 3:14. Akiwa angali mtoto Yesu alimjua babayake halisi, alipomwambia mamaye, ‘ hamkujua [yeye Yusufu] ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya baba yangu? (Luka 2:49).Mwishoni alipowaaga wanafunzi alisema “ nalitoka kwa Baba, name nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa baba” (Yohana mt 16:28)

4.     Wanafunzi wa Yesu Kristo  

(Mathayo 14:33 nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu)

5. Malaika wa Mungu                                                                                           

(Luka Mt 2:8-20 Wachungaji walipewa taarifa ya kuzaliwa kwa mtoto Yesu na Malaika wa Mungu)

 

6. Mapepo

Hata mapepo wanatambua ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na kwa asili mapaepo ni malaika waasi walikuwepo mbinguni ila wametimuliwa wanamjua Yesu maana walikuwa wakionana huko. (Mathayo 8:29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? Pia kwa habari ya kumjua Mungu na heshima mashetani wanamuheshimu Mungu mno kuliko sisi binadamu. (Yakobo 2:19 Wewe waamnini kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.)

Kwa kuongezea ni kwamba kila kitu kilichopo duniani original yake ipo mbinguni Magari ya duniani og yapo mbinguni, miili ya duniani og yake ipo mbinguni, kusifu na kuabudu kwa duniani kusifu og yake kupo Mbinguni, vyombo vya mziki vya duniani og yake vipo Mbinguni, Sauti za kuimba ya 1,2,3 na 4 og yake ipo Mbinguni, madini yote tunayo yajua og yake yapo Mbinguni swala la Mwana au baba tunakoitana duniani og yake ipo mbinguni, sauti na lugha og yake ipo Mbinguni na kadhalika.

Kwa hiyo Yesu sio Mwana wa Mungu kwa Mungu kuzaa na Mariam kama tulivyo kimwili kuzaliana sisi binadamu lazima kufanya tendo la ngono.  

Je tuukatae ushahidi wote huo wa maandiko waliomuona Yesu na kutuambia ushuhuda wao harafu tumsikilize, tumfuate Mtume Muhamad ambaye hata Yesu hamuamini na kumjua? Na kwa kutokumuamni kwake anaisubiria hukumu siku ya mwisho. Mtu yeyote asiye muamini Mwana wa Mungu, hukumu ya Mungu inamsubiri ni suala la muda tu. (Yohana Mt 20:30-31 Basi pia kuna ishara nyingine nyingi alizofanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa kwenye kitabu hiki lakini hizi zimeandikwa kusudi mpate kuamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na kwa kuamini mwe na uzima wa milele.

 Biblia inaposema kwa habari ya wana wa Mungu inamaana nyingine zifuatazo:

i.            Kwa Timotheo , mwanangu wa Imani (1Timotheo 1:2)

ii.         Heli wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu (Mathayo 5:9)

iii.       Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu (Warumi 8:14)

iv. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiowalwaliaminiojinalake. (Yohana Mt 1:12)

v.      Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. (1Yohana 3:9


Kwa nini wanapinga Yesu kuwa na Mwana wa Mungu?

(1Yohana2:18 watoto ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa  hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa Mwisho.)



TUKIO LINALO TEGEMEA KUTOKEA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA HAPA DUNIANI
·    Ujio wa Yesu Kristo mara hii itakuwa kwa nguvu si kinyonge kama alivyokuja hapo mwanzoni (Mathayo mt 24:27-30)

TUKIO LINALO ENDELEA KWA SASA HAPA DUNIANI
Roho Mtakatifu kufanya kazi/shughuli mbali mbali na kanisa lake kwa ajili ya kuliandaa,  (Warumi 8:28) na kuepuka mitego/hila mbali mbali ya Ibilisi anayoipanga kwa watu wa wote mf. ajali, maafa mbali mbali.

Wewe unayepinga uzazi wa Bwana Yesu na kutangazia uma wa watu usiku na mchana unampinga Mungu Yupi? Kama Mungu wako hawezi kitu, usimsemee Mungu wa wengine, usimsemee Yehova. Kwanza habari za Yesu hujui hata a, e,i,o,u yake . Hivi uliona wapi mtu hajui topic ya somo husika akaandaa muhadhara ili awaambie watu kuhusu hilo somo? Hivi kweli kwa mtu mwenye ufahamu wake atathubutu kwenda kusikiliza hapo mahali, hapo itakuwa ni kipofu anamwongoza kipofu mwenzake , itatokeaje kwao? (Luk Mt 6:39)
Mitume karibia wote walitabiri kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa jinsi uzazi wake utakavyokuwa  kwa jinsi ya ajabu, wewe ni nani hata upinge hayo, kama sio wale ambao biblia takatifu ilikwisha watabiri kuwa siku za mwisho kutatokea Manabii wa uongo. Sasa kwa taarifa yako endelea tena kwa bidii juhudi za kupotosha, ila nakutaadharisha isije ikatokea laana kwako nadhani utakuwa unapingana na mpango kamili wa Mungu wa wokovu kwa wanadamu wote, ambao Mungu Mtakatifu aliingia gharama. Tena kwa kujua au kutojua unashindana na Mungu muumbaji wa dunia hii wote watakao shindana na Mungu wasitegemee kupata ushindi ni kushindwa tu na laana itakayokuwa ikiwakalia wote na njama hizo za kupotosha zinazo fadhiliwa na mawakala wa shetani na wapinga kristo maana wapo wengi, na wataendelea kuongezeka.Na Shetani atakuruka siku ya siku maana hakukutuma ila umejituma mwenyewe atakucheka wakati ukiteswa na hukumu ya Mungu.

Huyo unayempinga ndiye atakaye kuja kuhukumu dunia hii na watu wote waliokufa na walio hai kutokana na matendo yao misahafu imeandika hivyo kwa kusoma na sio kwa kusomewa au kutafsiliwa na mwingine. Pamoja na kuwa ujio wa Yesu mara ya kwanza ilikuwa ya kinyonge sana, mara ya pili atakapokuja atakuja kwa nguvu kubwa itakayoifanya Dunia yote kupigwa na butwaa kufumba na kufumbua.

Shetani, mapepo yanamjua Mungu kuliko sisi binadamu kwa hiyo kwa kumjua Mungu huko hukutumia kuwapotosha binadamu tupotee mbali na uso wake na kuharibu uhusiano mzuri ambao Mungu anautaka toka kwa binadamu wote, Mungu hababaishwi na  dini, hata Shetani naye ana dini, yeye anachojua ni mahusiano mazuri (Utakatifu)

Ili kuilewa biblia inabidi uwe mmoja wa kondoo ukiwa nje hutaelewa utaishia kubisha tu na biblia ina lugha yake mf. Harusi ya mwana kondoo,maji yaliyo hai, kuzaliwa mara ya pili n.k  kilicho andikwa kimeandikwa, kuna lugha ya biblia ukiwa si muamini hutaelewa ngo, kama ilivyo kwa wanasheria wana lugha zao za kisheria, madaktari wana lugha zao ili kuelewa inabidi uingie ndani. Wachawi wana  lugha zao ukiwa si mchawi utatoka kapa.Wahuni wa vijiweni wana lugha yao ili kuelewa lugha zao inakubidi uingie ndani ujifunze ndio utaelewa bila hivyo utatoka kapa.

Kwa kuwa uzazi wa Yesu ndio msingi wa wokovu wote ukimpinga mtoto Yesu uzao wake utakataa kila kitu kinachomuhusu yeye utapinga miujiza, wokovu, kusurubiwa, kufufuka kwake na hata kurudi tena mara ya pili kwake na kwa kujua au kutojua utakuwa unapingana na Mungu na hapo kusudi la shetani la kutuchonganisha na Mungu litakuwa limekamilika.Wote wanaopinga uzazi wa Yesu, nawatahadharisha kuwa hili jambo kama litakuwa limetoka kwa mwanadamu mtafanikiwa kulipinga ila ikiwa limetoka kwa Mungu hamtaweza kulipinga, sababu mtakuwa mnapingana na Mungu. mtakuwa mkijitafutia laana, mikosi na mabalaa kwenu na vizazi vyenu. (Matendo ya mitume 5:38-39) Pia Mungu hashindani na mwanadamu hata siku moja na hata milele (Mwanzo 6:3)

Kama una nia umepanga kupinga uzao wa Yesu endelea kupinga, wokovu wake pinga, ujio wake mara ya pili pinga, na uwepo wa mbingu na kuzimu kuwepo pinga, sababu hata maandiko yanasema  maandiko hayapati shida na watu wa jinsi hiyo au vikundi vya watu wa namna hiyo kwani haviwezi kubadilisha hata nukta moja ya msahafu, pia na hukumu inawasubiri na inaweza kuanzia hapa hapa duniani, na shetani atakupinga maana yeye anamjua Yesu kwamba ni mwana wa Mungu aliye hai na ndiye atakaye kuja uhukumu ulimwengu tunaoishi sasa.Pia ujue ya kuwa aliyekupa pumzi ni Mungu huyo unayepinga mipango yake ya kumtafuta binadamu akae katika njia yake, pamoja na bidii ya shetani naye kutaka binadamu wasisikie habari njema za wokovu wakae hivyo hivyo. Injili itapenya tu kila mahali katika siku hizi za mwisho hakuna wa kuzuia mipango ya Mungu.

Ndio maana wengine wanaacha kutumia vitabu vya Imani zao wanatumia misahafu ya makafiri, kama fulani ni kafiri sio safi ni mchafu, hafai mbele za Mungu kwa nini utumie kitabu chake, soma chako au subiri usomewe na kutafsiliwa.Kama hutaki basi ujue na kuamini kuwa Mungu alizaa na anaweza kufanya jambo lolote hapa duniani sababu yeye anaweza yote na akiri za Mungu hazichunguziki, na hata akiri yetu sisi binadamu wote ni ndogo kumwelewa jinsi Mungu alivyo.

Kama utakuwa tayari kwa ajili ya maamuzi haya muhimu ambayo yatakusaidia sasa na hapo baadaye, tafuta mahali pa utulivu na usali sala ifuatayo iliyoandikwa ukimaanisha, baada ya sala tu utakuwa umesha mpokea huyu Yesu, na atakuwa Bwana na Mwokozi kwako sasa na milele.


“Bwana Yesu Kristo, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi sasa nageuka na kutubu na kuziacha dhambi zote nikimaanisha, niwezeshe kutozirudia kabisa na unijaze na Roho wako Mtakatifu aliye mwalimu na msaidizi wa kila mwamini. Pia nifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uniandike katika kitabu cha uzima wa milele. Asante Bwana Yesu kwa kuniokoa.Amen”


Kama ulikuwa ukisali sala hiyo hapo juu kwa kumaanisha, basi utakuwa umeshakombolewa, umeokoka.Kwa kuwa sasa umemwamini Bwana Yesu Kristo, vifuatavyo ni msaada kwako ili kusonga mbele.

1. Soma Neno la Mungu biblia takatifu kila siku. (Warumi 10:17), (Wakolosai 3:16)

2. Sali asubuhi mchana na jioni na kila ujisikiapo kufanya hivyo. (1Wathesalonike   5:17)

3. Kama sehemu unayomwabudu Mungu hawaamini Biblia Takatifu tafuta kanisa linalokiri  wokovu na      kutoa mafundisho ya kiroho upate kuukulia wokovu. (1Petro 2:1-2), (Waebrania 10:25)

4.  Fanya kazi kwa bidii na uaminifu,jitume usione aibu, acha uvivu, tafuta pesa, Mungu katoa                         agizo tangu kale, Yeye alifanya kazi, Yesu alifanya kazi, mitume vivyo hivyo,   (2Thesalonike                       3:10)

5. Usikubari kusikiliza uongo wa Shetani. (Ufunuo 3:11), ( Mwanzo 3:1-19) (1Petro 5:8)

6. Sambaza ujumbe huu kadri uwezavyo, na Mungu atakuongezea kitu, huwezi kujua nani anahitaji ujumbe kama huu siku hii ya leo.(Ufunuo 22:18) ,( Kolosai 4:16)

                                                                            Ni mimi

Mtumishi Emmanuel T.M.Omari
injiliyajioni@gmail.com
www.injilijioni.blogsport.com









No comments:

Post a Comment