1. Aliigawa bahari ya Shamu watu wakapita kati kati yake (Zab 66:5-6)
2. Mungu aliwahi amuru mwanamke wa miaka 90 azae mtoto ikafanyika hivyo (Mwanzo 21:2)
3. Mungu aliwahi ruhusu punda mnyama aongee sauti ya kibinadamu kitu ambacho hakitegemewi kabisa (Hesabu 22:28-30)
4. Mungu aliumba nyota ,mwezi, jua vingine vinavyo onekana ambavyo bado kugunduliwa na visivyo onekana.
5. Mungu aliwahi kuiangamiza dunia yote kwa maji na kubakisha watu nane tu walio mpendeza moyo wake.(1Petro 3:20)
6. Mungu aliwahi simamisha Jua kwa muda (Yoshua 10:13)
7. Mungu aliwahi kuingilia mawasiliano ya mtu na mtu wasielewane ili kusudi lake litimie.(Mwa 11:1- 9)
8. Mungu anaweza fanya mvua inyeshe katika nchi na mafuriko yakatokea, pia anaweza ruhusu mvua isinyeshe na kukatokea ukame katika nchi yoyote aitakayo yeye.(1Fal 18:1)
9. Mungu anaweza kufanya muujiza wa samaki wawili na mikate mitano wakala zaidi ya watu 10,000 watu wakala wakashiba na kuisaza.(Yoh Mt 6:1-13)
10. Mungu anaweza amuru jabari/jiwe kubwa litoe maji ikafanyika hivyo (Hesabu 20:8 -11)
11. Mungu anaelewa lugha zote za hapa duniani, hata lugha za wanyama, ndege,miti, bahari ,wadudu etc (Zab 96::11-12), (Zab 98:7-8)
12. Kwa uweza na nguvu zake anatawala milele yote kwa haki tena ni mtakatifu mno mfano wake duniani, mbinguni hakuna. (Zab 66:7)
13. Mungu aliwahi kumfufua Yesu aliyekuwa amekufa, Lazaro naye alifufuliwa tena alikuwa ameshaanza kuoza na kunuka (Mark 8:31)
14. Alimgeuza jambazi sugu Paulo aliyekuwa akiitwa Saul kutoka katika ufalme wa giza na kumuingiza katika ufalme wa nuru yaani wa Yesu Kristo.(Mdo 9:1-22)
15. Mungu huyo huyo anaweza kumtumia mtu mwingine unayemdhania kuwa hafai, taka taka, kafiri kukuletea habari za ukombozi wa roho yako ukikubari ni kwa faida yako na ukikataa pia ni kwa hasara ya nafsi yako (1Kor 1:27)
16. Mungu aliwahi ruhusu ardhi ifunue kinywa na kufumba iwameze wale walio mkosea kitu ambacho ukifikiria kwa akiri ya kawaida akiingii akirini, unashindwa kuelewa kabisa.(Hes 26:10)
17. Mungu ana uwezo wa kukuona wewe usimuone, pia ana uwezo wa kurekodi matendo yako yote mabaya na mema na kuyaweka katika CD yake ya ki ungu na kuyatumia kama ushahidi wa siku ile ya hukumu itakapo fika.Hata jiwe linaweza kutoa ushahidi kwa Mungu (Yoshua 24:27)
18. Mungu ana uwezo wa kuruhusu ushirika wa mwanamke na mwanaume azaliwe mtoto, kwa nguvu na uwezo wake, pia anaweza ruhusu mwanamke azae bila ushirika wa mwanaume kama ilivyo kwa bikira Mariamu (Mathayo 1:23/ Isaya 7:14) Ni kamuujiza cha mtoto mbele za Mungu.Mamaye Yesu pia aliuliza litakuwaje jambo hili wakati sijui mume…? Malaika/Mungu baada ya kujieleza mwisho kasema hakuna jambo la kumshinda Mungu, pia maana yake ni Mungu anaweza kufanya lolote atakalo, hashindwi na lolote. Hapa inamaliza maswali yote ya inawezekanaje kuzaa bila mwanaume, kwa mwelewa.(Luka mt 1:34-38)
19. Aliokoa na anaendelea kuokoa kila siku watu wa Imani zote ambao walikuwa hawamjui Yesu baada ya kuujua ukweli wa Wokovu (Waebrania 3:7-8)
20. Mungu pia haimtishi iwapo idadi kubwa ya binadamu/watu wataamua kwa hiyari yao ku tomfuata Yesu jina litupasalo kuokolewa kwalo wenyewe na kumfuata mfalme wa anga Shetani na mwisho kuangamia katika moto wa jehanamu. (Mwa 9:3) Alishawahi kuiangamiza Dunia na kuua watu wote kwa Gharika na kubakisha watu nane tu, pamoja na watu kulia na kusaga meno haikusaidia.
21. Mungu halali hasinzii akitulinda, pamoja na ukaidi wetu, wakati sisi binadamu hulala, husinzia, tunapolala adui ni rahisi kutuvamia ni ulinzi wa Mungu tu utupao uzima siku hadi siku (Zab 121:3-5) Ayu 1:7-10)
22. Katika ulimwengu tunaoishi kuna nyota nyingi mabilioni kwa mabilioni lakini Mungu zote azijua tena kwa majina na idadi ya nywele za vichwa vyetu vyote inajulikana, binadamu duniani tupo wangapi? (Luk 12:7) (Zaburi 147:4)
23. Mambo aliyofanya Mungu na anayotufanyia sisi binadamu ni mengi mno hayaandikiki katika karatasi yakatosha hayahesabiki (Yoh 21:25) ingawa Shetani kwa dharau zake kwa Mungu anashawishi binadamu wayaone yote aliyofanya Mungu ni maajabu saba ya dunia. Hakuna maajabu saba ya dunia kuna maajabu zaidi ya maelfu ya Mungu sio ya dunia ni ya Mungu Mtakatifu, unapotaja Mungu unakuwa umemsifu Mungu, unapotaja dunia unakuwa umemsifu mungu wa dunia.
24. Mbingu ni kiti chake cha enzi, duniani ni mahali pa kuweka miguu, Ukuu wa Mungu umepita ufahamu wa binadamu (Isaya 66:1)
25. Mungu mbingu hazikutoshi wala mbingu za mbingu. Ewe mwanadamu kwa akiriyako utamlinganisha na kitu gani, kama si kumwacha tu Mungu aitwe Mungu.(2Nyakati 6:18)
Mungu akipa kila kiumbe chakula chake, ulimwenguni hapa kuna viumbe vingapi? (Zab 136:25) Unataka kumfananisha na nani hapa duniani? Na Rais yupi, tajiri yupi, mfalme yupi?
BAADHI YA SABABU KWA UCHACHE, KWA NINI YESU NI
MWANA WA MUNGU KWA USHAHIDI WA MAANDIKO
1.
Manabii
Walitabiri walitabiri kuzaliwa kwake
kabla (Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa
miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atatokea mmoja...), (Mathayo Mt 2:6 Nawe Bethlehemu,
katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; kwa kuwa kwako
atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israel) , (Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana
mwenyewe atawapa ishara.Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume,
naye atamwita jina lake Imanueli) (Mathayo
1:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za
mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sharia, yaani, adili,
na rehema,na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.)
Mungu ana utaratibu wa kuwajulisha rafiki zake, baadhi ya mambo kabla ya
kuyafanya (Mwanzo 18:17 Bwana
akanena Je! Nimfishe Ibrahimu jambo nilifanyalo, ; (Amosi
3:7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi
wake manabii siri yake) (Yohana
mt 15:15 siwaiti tena watumwa kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake;
lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu
nimewataarifu. Hakuna msingi thabiti wa Imani kama wa Manabii na Mitume (2Nya 20: Wakaamka asubuhi na mapema …
(Waefeso 2:20 Mmejengwa
juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la
pembeni)
2.
Mungu mwenyewe, Petro, Yohana na Yakobo
(Yohana mt 3:16 Kwa
maana jisi hii ungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee.)
(Mathayo 17:15 Alipokuwa katika kusema, tazama
wingu jeupe likawatia uvuli ; na tazama sauti ikatoka katika lile wingu,
ikasema, Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni
yeye).
3.
Yesu mwenyewe
(Yohana Mt 10:36 Je! Yeye ambaye Baba alimtakasa,
akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru? ; kwa sababu nalisema , Mimi
ni mwana wa Mungu? Naye akajibu ni nani? Ni nani, Bwana, nipate
kumwamini? Yesu akamwambia, umemuona, naye anayesema nawe ndiye. Sio
hivyo tu bali Yesu mwenyewe alikiri kuwepo kabla ya kuzaliwa duniani
aliposhiriki utukufu wa Mungu (Yohana mt
17:5 tena alisema, kabla babu yake
Ibrahimu kuweko alikuweko alikuweko kama niko ambaye niko (Yohana Mt 8:58, Kutoka 3:14.
Akiwa angali mtoto Yesu alimjua babayake halisi, alipomwambia mamaye, ‘
hamkujua [yeye Yusufu] ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya baba yangu? (Luka 2:49).Mwishoni alipowaaga
wanafunzi alisema “ nalitoka kwa Baba, name nimekuja hapa ulimwenguni; tena
nauacha ulimwengu; na kwenda kwa baba” (Yohana mt 16:28)
4.
Wanafunzi wa Yesu Kristo
(Mathayo
14:33 nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u
Mwana wa Mungu)
5. Malaika wa Mungu
(Luka Mt
2:8-20 Wachungaji walipewa taarifa ya kuzaliwa kwa mtoto Yesu na Malaika wa
Mungu)
6. Mapepo
Hata mapepo
wanatambua ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na kwa asili mapaepo ni malaika waasi
walikuwepo mbinguni ila wametimuliwa wanamjua Yesu maana walikuwa wakionana
huko. (Mathayo 8:29 Na
tazama, wakapiga kelele, wakisema, tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je umekuja
kututesa kabla ya muhula wetu? Pia kwa habari ya kumjua Mungu na
heshima mashetani wanamuheshimu Mungu mno kuliko sisi binadamu. (Yakobo 2:19 Wewe waamnini kuwa Mungu ni
mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.)
Kwa
kuongezea ni kwamba kila kitu kilichopo duniani original yake ipo mbinguni
Magari ya duniani og yapo mbinguni, miili ya duniani og yake ipo mbinguni,
kusifu na kuabudu kwa duniani kusifu og yake kupo Mbinguni, vyombo vya mziki
vya duniani og yake vipo Mbinguni, Sauti za kuimba ya 1,2,3 na 4 og yake ipo
Mbinguni, madini yote tunayo yajua og yake yapo Mbinguni swala la Mwana au baba
tunakoitana duniani og yake ipo mbinguni, sauti na lugha og yake ipo Mbinguni
na kadhalika.
Kwa hiyo
Yesu sio Mwana wa Mungu kwa Mungu kuzaa na Mariam kama tulivyo kimwili
kuzaliana sisi binadamu lazima kufanya tendo la ngono.
Je tuukatae
ushahidi wote huo wa maandiko waliomuona Yesu na kutuambia ushuhuda wao harafu
tumsikilize, tumfuate Mtume Muhamad ambaye hata Yesu hamuamini na kumjua? Na
kwa kutokumuamni kwake anaisubiria hukumu siku ya mwisho. Mtu yeyote asiye
muamini Mwana wa Mungu, hukumu ya Mungu inamsubiri ni suala la muda tu. (Yohana Mt 20:30-31 Basi pia kuna ishara nyingine
nyingi alizofanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa kwenye kitabu
hiki lakini hizi zimeandikwa kusudi mpate kuamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu
na kwa kuamini mwe na uzima wa milele.
Biblia inaposema kwa habari ya wana wa Mungu inamaana nyingine zifuatazo:
i. Kwa
Timotheo , mwanangu wa Imani (1Timotheo
1:2)
ii. Heli
wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu (Mathayo 5:9)
iii. Kwa
kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu (Warumi 8:14)
iv. Bali
wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiowalwaliaminiojinalake. (Yohana Mt 1:12)
v. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. (1Yohana 3:9)
Kwa nini wanapinga Yesu kuwa na Mwana wa Mungu?
(1Yohana2:18 watoto ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa Mwisho.)